WHY YOU? (KWANINI WEWE?)
Imeandaliwa na Joche kutoka JocheApp.
Nakusalimu ndugu msomaji wa makala zetu za JocheApp.
Usisahau kudownload Application yetu katika simu yako inapatikana mwa jina la JocheApp katika Playstore (Adroid) yako.
Katika maisha tunatembea na kukutana na vitu vingi na watu wa aina mbalimbali wenye mitazamo na fikra tofauti tofauti lakini pia wenye viwango tofauti vya maisha.
Katika pita pita zangu za harakati za maisha nikiwa katika mgahawa mmoja nikawaza hili swali la WHY ME/YOU ndipo nikaona nikutafakarishe na wewe kidogo katika jambo hili.
Kwa mfano:
1. Una biashara unataka kuuza vitu, swali la kwanza kwanini ni nunue kwako na si mtu kwingine????
Kwanini wewe?
2. Unataka wawekezaji kwenye biashara yako? Ambao wataweka pesa zao na ili waweze kupata faida katika kuwekeza kwako na wewe pia biashara yako ikue?
Swali la kujiuliza:
Kwanini wewe??
3. Umetafuta kazi na unavyo vyeti sawa na wakati mwingine unamadaraja mazuri ya ufaulu (other things remain constant).
Jambo la kujiuliza
Kwanini mwajiri akuajiri wewe na si mwingine?
4. Hebu tutazame upande wa pili...
Sote tunamwomba Mungu aweze kutufanikisha. Yaani kila mtu anatamani Mungu amvushe kwenye madaja ya juu iwe ki-huduma au kimwili au hata kifedha.
Swali:
Kwanini akujibu wewe na mwingine abaki pale alipo au ajibu sawa sawa na uombavyo na mwingine kwa namna nyingine?
5. Mimi na wewe ni marafiki lakini pia tuna marafiki wengi sana. Tunafanya mambo kadha wa kadha pamoja.
Vipi ukiwa na jambo lako ukalileta kwangu na mwingine pia akawa na jambo kama hilo hilo.
Swali:
Kwanini nikusaidie wewe na nimuache mwingine?
Ni mambo mengi sana ambayo unaweza kujiuliza kwanini wewe na sio yule au kwanini mimi na sio wale?
Ukifika kiwango cha kujiuliza SWALI HILI katika mambo kadha wa kadha kuna vitu utagundua ni vidogo lakini vina mantiki kubwa sana kwa maisha ya mwanadamu.
Kufahamu tu jina langu JOCHE or BERNALD haitoshi, kuwa na namba yangu ya SIMU haitoshi, kufahamu ninapoishi haitoshi kusema sisi ni marafiki lakini pia kuwa marafiki tu haitoshi kuna vitu ambavyo huongeza na kuweka utofauti kati ya rafiki A na rafiki B.
*JocheApp*
____________________________________
Author: Joseph G. Mrema
Contacts: 0712 851687 (whatsapp only)
Email: josephgeotham4@gmail.com
15th/October/2018
____________________________________
Kuna zaidi ya hapo.
*Nikutakie TAFAKARI NJEMA SIKU YA LEO*
No comments
Post a Comment