UNA FAIDA GANI?

Una faida gani kwangu?
Ukiwa kama mpenzi wangu una faida gani kwangu?

Ukiwa kama mke wangu una faida gani kwangu?

Ukiwa kama mume wangu una faida gani kwangu?

Ukiwa kama rafiki yangu una faida gani kwangu?

Mimi nina faida gani kwako?

Unanufaika na nini kwa kuwa na mimi?

Naanza na mfano wa kampuni. 
Assume unataka kufanya kazi kwenye kampuni Fulani,kisha unauliza :
Hebu niambieni benefit programs za kampuni yenu?
Kampuni itaanza kutaja;
“hizi ni benefit programs tulizonazo, tunawapa wafanyakazi bima ya Afya, tunawapa wafanyakazi nafasi ya kusoma baada ya muda Fulani, tunawapa wafanyakazi nafasi ya kushare faida ya biashara yetu nk”
Ukisikia faida za kufanya katika kampuni kama hiyo, unafurahia kuingia katika kampuni hiyo kwasababu ya faida zake. 

Swali kwako sasa?
Wewe una benefits program gani kwenye kampuni?
Wewe una faida gani kwenye kampuni?
Mtu unaamka asubuhi na CV ya kukopi na kupaste unatafuta kazi, ukiulizwa nini faida ya wewe kwenye kampuni hujui. Unatafuta kazi ya nini sasa?

Turudi kwenye maisha. 
Nitapata faida gani kwa kuwa rafiki yako?
Nitapata faida gani kwa kuwa mpenzi wako?
Naomba nikuulize swali leo; 
“Ikitokea mtu akawa karibu na wewe , je atafanikiwa kimaisha au atarudi nyuma kimaisha?”
“Ikitokea mwanaume akawa mpenzi wako leo, je atafanikiwa kimaisha au atarudi nyuma kimaisha?”
“Ikitokea mwanamke akawa karibu na wewe, je atafanikiwa kimaisha au atarudi nyuma kimaisha?”

Unaweza kutaja watu wawili, watano, kumi na zaidi waliowahi kuwa karibu na wewe na wakafanikiwa kimaisha kwasababu ya faida ya kuwa na wewe?

Ukiwa kama mwanamke ni nini faida yako kwa mpenzi wako zaidi ya sex?

Ukiwa kama mwanaume ni nini faida yako kwa mpenzi wako zaidi ya sex?

Una faida gani kwa wengine? Wewe ? 
Una faida gani kwa mpenzi wako? Wewe?
Au ni chuma ulete tu?

Una faida gani kwa mume wako? Wewe?
Una list ya watu walionufaika kupitia wewe?

Kuna marafiki ambao ukiwa karibu nao utanufaika kwa network za kibiashara.

Kuna marafiki ambao ukiwa karibu nao utanufaika na mawazo makubwa ya kimaisha.

Kuna marafiki ambao ukiwa karibu nao utanufaika kwa kukutana na wadada wazuri na kuponda mali zako.

Kuna wadada ambao ukiwa karibu nao utaishia kula mpaka mtaji wa biashara yako.

Kuna wadada ambao ukiwa karibu nao utaishia kupoteza muda na mwelekeo kwasababu hawana hata mawazo ya kukusogeza mbele.

Kuna marafiki ambao ukiwa karibu nao utaishia kuwa mchangiaji wa michango ya harusi.

Ninawajua watu waliokuwa na mwelekeo mzuri kwenye maisha, lakini walipooa wakapoteza kila kitu. 

Ninawajua watu waliokuwa hawana kitu wala mwelekeo walipooa wakabadilika na kuwa wenye maisha makubwa.

Ninawajua watu walioingia kwenye mapenzi , ndani ya muda Fulani wakajinyonga.

Ninawajua watu walioanza urafiki na mwisho wake wakasimamisha biashara kubwa pamoja.

Swali ni lile lile- ni nini faida ya kuwa karibu na wewe?
Mimi nitanufaika nini nikiwa na wewe?
Una faida gani kwenye familia yako?
Una faida gani kwa mpenzi wako?
Una faida gani kwa ndugu zako?
Una faida gani kwa watoto wako?
Una faida gani kwenye Nchi yako?
Tanzania inanufaika na nini kwa uwepo wako?
Mkoa wako unanufaika na nini kwa uwepo wako?
Una faida gani wewe?
Narudia tena what benefits programs do you offer to others?

Geophrey Tenganamba,
#Fursa 101
—————————————————
JocheApp

1 comment

Unknown said...

Thank you for sharing

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...