MAKUSUDI YA KUFANYA HILO UFANYALO NI NINI?
Kwenye kila hatua ya maisha yako kuna vitu utakuwa unafanya kwa SABABU MBALIMBALI..
Kwanza, kuna yale mambo ambayo utayafanya kwa sababu unataka “EXPOSURE”.
Kwenye hili unataka KUONESHA ulichonacho.
Hili ni muhimu, kwa sababu ukiwa na kitu KIZURI ila hakuna ANAYEKIJUA ni Sawa na KUTOKUWA nacho.
Pili, unaweza kufanya kwa sababu ya “CONNECTION”...
...Yaani unataka ufahamiane na mtu fulani ambaye unajua atakuwa na faida fulani huko mbele.
Katika hatua hii, unaweza kugharamia kwenda MAHALI au kufanya kitu...
...sio kwa sababu unalipwa, ila tu UFAHAMIANE na mtu fulani.
Tatu, kuna wakati unafanya vitu kwa ajili ya PESA tu.
Yaani lengo kubwa hapo ni Kutoa THAMANI fulani ili ULIPWE kiasi fulani.
Kwenye hatua za maisha yako kuna wakati unaweza kufanya kwa ajili ya kimojawapo tu...
...au kwa ajili ya viwili au kwa ajili ya vyote VITATU.
Kikubwa ni kuelewa, kwa chochote unachofanya kwa wakati huo, UNATAFUTA NINI?
Nakutakia MAFANIKIO MAKUBWA.✍🏾
No comments
Post a Comment