UNAJIONA KATIKA KIWANGO KIPI?
Sehemu 1
Ukiaminiwa na ukahisi unaaminiwa na watu chunga sana mienendo yako hasa unapokuwa hauko nao karibu, maana kwa kusikia kwao habari zako.
Watatumia kama moja ya kigezo cha kuanza kukufuatilia kwa ukaribu na kutamani kujua je ndivyo ulivyo au ni maneno tu ya watu.
Uaminifu wako kwa matendo sio kwa maneno unaweza kusogeza fursa nyingi mpaka zile ambazo zisizo nje ya uwezo wako au usizozitegemea na kutoka kwa watu ambao usio wategemea na utakutanishwa na watu kadha wa kadha ambao wanaweza kusogeza mambo yako kwa hatua moja, mbili na mpaka kumi kwa wakati mmoja.
Watu wengi hudhani kwa kufanya mambo yasiyo mema kwa watu wasiowajua basi hakutadhuru au kuleta madhara kwenye maisha ya watu wanaowajua. Dunia kwa sasa imekuwa zaidi ya kijiji.
Una maono ya kwenda mbali. Ni kweli tutasema anza na ulipo. Lakini kumbuka kuna vitu vidogo vidogo ambavyo vinaweza kukukwamisha kusogea mbele.
Kwa namna ambavyo utahangaika na kazi ya mtu mwenye deal la 10milion basi unadhifu huo huo, na speed hiyo hiyo, na ubora huo huo, na uaminifu huo huo na nidhamu ile ile iwe hata kwa mtu ambaye amekuja na deal la 10,000.
Usibague kuonyesha kiwango cha ubora kutoka na jinsi mtu alivyo, au ukubwa wa kazi akupayo, au aina ya kazi aliyokupa. Maana hujui nani utakutana nae, nani yuko nyuma yake, nani anakutazama.
TUJIFUNZE UAMINI NA UBORA KILA IITWAPO LEO.
Itaendelea........
Joseph Mrema.
No comments
Post a Comment