USTAARABU

Hi! Guys,

Ustaarabu ni kitu cha muhimu sana katika maisha. Ustaarabu ni pale unapoweza kuheshimu wenzako, kujiheshimu wewe mwenyewe, kuwa humble na kuwa na moyo wa kusaidia pale unapoweza/unapohitajika. Ustaarabu unakufanya watu wakuheshimu, wakupende na pia unakufanya uwe mtu wa maana. Kuna mambo madogo madogo sana ambayo watu wanafanya na wanaona ni mambo ya kawaida wakati sio ya kawaida. Mfano:

—Mtu kakuazima kitu utumie, kwa nini usikutunze kama chako? Kwanini ukirudishe kikiwa kimeharibika? Au kichafu? Au kutokurudisha kabisa?

—Umekuta sehemu uliyokaa ni safi, kwanini usiiache ikiwa safi? Hata kama ni chupa tupu ya maji, gum, maganda ya pipi, huo ni uchafu. Watu wengine wana tabia ya kutupa uchafu hata mbele ya nyumba za wenzao. Why though?

—Mwenzio kakuomba mkutane sehemu fulani saa fulani, kwanini uchelewe? Au kwanini umdanganye kuwa upo karibu wakati sio ukweli? Au kwanini umwambie utafika halafu usifike bila kutoa taarifa? Kutoa taarifa ni kitu muhimu sana. Upo stuck kwenye foleni, mwambie mwenzio utachelewa au wahi kutoka unapotoka. Hutafika mjulishe mwenzio huji tena. 

—Mwenzio kakukosea, kwanini usijaribu kuongea naye kwa upole. Kama hataki, its his or her loss. Samehe uende zako. Sio lazima uanze kumtukana au kumsema kwa watu wengine. 

—Sawa, labda wewe unakipaji fulani. We get it. Tumia kipaji chako vizuri. Sio lazima wengine wataabike kwa sababu yako. Fanya sehemu yako, wape na wengine chance ya kufanya sehemu zao. Sio kila kitu wewe ndio mjuaji na pia maringo huwa hayasaidii, watu watakudharau.

—Ujifunze kusema maneno kama “asante”, “samahani”, “tafadhali” n.k. Usiwe ni mtu wa kucommand (kuamrisha) unapotaka kitu. Usiwe mtu wa kulalamika tu katika kila kitu. 

—Umealikwa sehemu ukaambiwa uje mwenyewe, wewe unabeba ukoo mzima. Hujui kule mwenzio kajiandaa vipi. 

—Umesikia kitu fulani kinachomhusu mtu fulani, hivi ni lazima uanze kupeleka maneno kwa watu wengine? Tafuta muda wa kuongea na mhusika kama hicho kitu kitamletea madhara. Au watu wawili wamegombana, wewe ndio unakuwa wa kwanza kuwa mchonganishi. Jifunze kuwapatanisha watu sio kuchanganisha. Jifunze kunyamaza kimya pasipokuhusu.

Kuna mambo mengi tu siwezi mention yote.

Mtu mmoja aliniambia kuwa kuna vitu ambavyo vinafanya sometimes watu wanakosa ustaarabu ila sio kwamba hawataki kuwa wastaarabu. Sisi ni binadamu so hatupo perfect na tunadeal na watu sio malaika. Akanipa scenarios kama, what if umepata accident huwezi toa taarifa muda ule or what if mtu umemsubiri muda mrefu sana halafu ukaishia kukasirika n.k. 

Na mimi nataka kusema nakubaliana naye kabisa. Mambo mengine hatuna control over ambayo yanatufanya tusionekane wastaarabu. Maisha yetu kila siku kuna changamoto mbalimbali. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, “Do your part and do not worry about the things you have no control over”. Utakuja kuelezea na kutoa apology later when you can. If huyo mtu unadeal naye ni mtu mzuri, atakuelewa.

Kitu kimoja nachotaka kuweka clear pia ni kwamba kuchagua kuwa mstaarabu sio ndio kwamba unawoga fulani au ni unafiki. What am saying is, “Do good and be good for no reason, sensible people will always appreciate”. Usifanye kitu kwa woga, fanya kwa kuwa unafikiri kuwa hiki kitu ni kizuri, unapaswa kufanya na wala hakiwezi kukuletea madhara yoyote mabaya.

Usipende kufanya kitu ambacho hupendi kufanyiwa. Uwe na uchungu na kitu cha mtu, uwe na uchungu na wenzio. Wao pia wanaumia kwa vile unavyotenda. Huenda wewe unaona jambo ni dogo lakini kwa mwenzio ni kubwa sana.

May be the statement "it all starts with you" is not reality. Lakini mimi nauhakika kuwa kila mtu akiamua inawezekana, maana watoto wake/familia yake watajifunza kwake. That is how it works. Sawa labda jirani/colleague n.k sio mstaarabu, kwanini labda wewe uache ustaarabu wako na kuwa kama yeye? Be the bigger person and take the higher road. 


----------------------------------------------------------------------------------------------------

Author: Rachel Stephen

Joche Inspirational and Motivational Inc

Follow Us:
Fb: Joseph Geotham Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Fb Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com

Contacts Us:
Whatsapp & Calls: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...