UNATUMIAJE AKILI YAKO?
Habari za wakati huu mwanaharakati nilitambua nankuthamini harakati zako za kutengeneza maisha na kufikia malengo yako nakupa Hongera....
Siku ya leo natamani sana kukazia jambo ambalo ni muhimu pia katika kuelekea ndoto zetu za kilele cha maisha yetu....
Katika vitabu vitakatifu tunajifunza imani chanzo chake ni kusikia...
Hilo ni kweli halipingiki kwa kadiri ya mambo unalisha roho yako na moyo wako ndio hayo yatakayokutoka....
Je katika siku ya leo umesikia mangapi???
Mangapi yanakazia juu ya ww kufanikiwa au kusonga mbele zaidi?? Au kutokukata tamaa???
Je Ubongo wako umeulisha jambo gani?? Au tumekazana na tumbo tumesahau ubongo/akili???
Mwanafalsafa mmoja akasema
"Akili ya mwanadamu ni kama Parashuti.."
Akimaanisha kwamba kama usipolifungua PARASHUTI urukapo toka angani halitakusaida daima na utadondoka nalo mpaka chini na kupasuka vipande vipande lakini ukilifungua basi litakusaidia na kuokoa maisha yako ....
Nini maana yangu?
Akili yako ukiipa kazi itakusaidia na itakuvusha kwenda kiwango kingine lakini ukiilalia haitakusaidia hata siku moja....
Ongeza ufahamu kila iitwapo leo vitabu vipo vingi sana..
Simu yako ni maktaba kubwa sana unaweza jifunza kila siku...
Usiridhika na jambo moja unalolifahamu...
Kaza mwendo safari bado ni ndefu...
Usikubali kufikia mwisho wa maisha yako bila kuacha alama humu ulimwenguni, bila kubadili mfumo wa maisha yako...
Mafanikio ni zaidi ya mapambano maana kila siku changamoto mpya ambazo zinataka maarifa mapya....
Kila siku huwa nakazia sana swala la mtu kuanza hapo ulipo.. Usingoje mpaka aje fulani au upate mtaji wa kiasi fulani.. Fursa huwa hazina hodi.. zinakuja wakati wowote na mahali popote...
Usiogope fulani atakucheka au atakuona hujaelimika.
JE WAJUA???
1.Ukianza watakucheka
2. Wakiona unaendelea bila kukata tamaa watakuja kutazama nini unafanya na wengine watakuunga mkono na kukosoa kwa kila aina kwanini usifanye hivi au fanya vile, au mbona bei fulani au fulani alifanya hivi..
3. Wakiona huwasikilizi wataanza kukudharau kuwa utafeli....
4. Ukiaanza kufanikiwa wataanza kukupinga na wengine watakusogelea uwe rafiki yao....
Hivyo usiyumbishwe na mwonekano wa nje wa dunia hii angalia ndani yako unataka nini..........
Nikutakie wakati mwema
_________________________________________________
Author: Joseph Geotham Mrema
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc
Follow Us:
Fb: Joseph Geotham Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Fb Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com
Contacts Us:
Whatsapp & Calls: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com
No comments
Post a Comment