SAFARI NI YAKO MWELEKEO NI WAKO

Habari ndugu msomaji wangu???

Napenda kuwasalimu wanaharakati na wapambanaji wa kuhakikisha wanaishi katika maisha yale wanayoyataka na kuyatamani....

Ni wakati mwinginr tena nakukaribisha katika mfululizo wa makala zetu ambazo mlengo mkuu ni kukutia moyo na kukuongezea hari na shauku ya kufika pale unapotaka kufika lakini pia kukuelimisha na kukupa chachu katika kahakikisha tunafika katika lengo lile tunalotaka...

Maisha ni safari...

Huu ni msemo ambao wengi tunaufahamu na tumezoea kuutumia kuna mabonde na milima na tambarare....

Kama zilivyo safari nyingine, lazima kuna mahali unaanzia na kuna mahali unaelekea na aina ya usafiri utakaotumia pia waujua wewe ambaye uko na safari....

Mfano anayeenda Mwanza akitokea Dar es Salaam safari yake na maandalizi ya safari yake ni tofauti na mtu anayetoka Ubungo anaenda Manzese au anaenda Mwenge.... 

Maandalizi yao ya safari ni tofauti, Mwendo wa Safari ni tofauti, Umbali wa Safari ni tofauti, Nauli ya safari ni tofauti, changamoto na magumu ya safari hayafanani kabisaaaa.......



Swali la Msingi: Wewe safari yako ya maisha ni unaekekea wapi????

Ukijua unapoelekea hutaangalia safari ya mwenzio, hutaangalia maandalizi ya mwenzio, hutajilinganisha na changamoto za mwenzio....

Lazima utakuwa na mwelekeo wako ambao unakupelekea katika kufika kule unapoenda.....

Na ukishajua safari yako na upande unaoenda utashangaa wale wenye dira na mwelekeo unaofanana na wewe utawapata na wale wanaokudandia watakukimbia maana mwendo wako hautafanana na wakwao, speed yako haitafanana na yakwao, maandalizi yako hayatafanana na yakwao, changamoto zako hazitafanana na zakwao......

Ulinganifu wa Umri, ufanano wa Jinsia, urafiki, undugu, kiwango cha elimu hivi vyote haviwezi kukuzuia kufanya jambo la kuibadilisha dunia yako.... 

Halafu jambo la kukumbuka kuwa kiwango cha mafanikio yangu hakiwezi kufanana na kiwango chako, ndio maana wapo ambao akipata pikipiki kwake ndio ameshafanikiwa na ndoto yake imeishia hapo, lakini wapo ambao wanatamani kumiliki ndege ndio ataona amefanikiwa...

Sasa speed ya hawa watu wawili lazima iwe tofauti tu, namna ya kupambana lazima itifautiane tu, matumizi ya muda lazima yatofautiane tu..

Nikukumbushe: Mapambano ya kufikia ndoto zako yanakutaka wewe... yanataka ukubali kubadilika na kuanza kufanya mambo ambayo unaona hayawezekani ndio utakapoweza kuvuka lakini ukiendelea kufurahi kufanya yake ambayo kila siku unayafanya badiliko litakuwa ni dogo sana na speed yako itakuwa ni ndogo sana katika safari yako ya mafanikio yako.....

Uwe na wakati mwema... 

Kwa Makala nyingine zaidi karibu....

www.jocheinc.blogspot.com
_________________________________________________

Author: JOSEPH GEOTHAM MREMA
CEO and Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc

Visit Us
Facebook: Joseph Geotham Mrema
Tweeter: Joseph G. Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Fb Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com


Contact Us:
Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp&Calls: +255 (0) 712 851 687

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...