KWANINI NI MUHIMU KUSEMA HAPANA (NO)

Neno NO ni neno fupi sana lakini madhara yake ni makubwa sana katika mafanikio yako au kushindwa kwako... Hivyo basi napenda kukukaribisha katika makala hizi zinazokujia kwa lengo la kukusaidia kuongeza maarifa na kuboresha maarifa yako pia...

NO ni neno lenye herufi mbili tu lakini linamadhara makubwa sana katika maisha yetu (madhara chanya na madhara hasi)...endapo ukifahamu muda na mahali pa kulitumia basi hutapata shida wala hutaona ugumu katika maisha

Maisha yetu binadamu yamegubikwa na vipindi vya aina nyingi, ambavyo vipindi hivi huleta furaha na muda mwingine huzuni....

Lakini katika hali zote hizo hutegemea na ni vip tunazitumia NO zet katika maisha yetu

Siku ya leo nimetamani kuongea na wewe mwanaharakati hasa juu ya uhitaji wa kujifunza kusema NO au HAPANA..

Mfano: Unapoona jambo linapofanyika linakuumiza au halina faida kwako ni muhimu kusema NO kwa jambo hilo.. 

Lakini ukifanya ili kumridhisha mtu matokeo yake yatakupata wewe ambayo uliyaona si mazuri... Lets learn to say NO.

Kwa kusema huku NO.. unaweza fanikiwa katika maisha yako au kukwama.. 

Uonapo fursa ukaiona inawalakini katika hatua za mwanzo lakini ukalazimisha tambua mwisho wake athari zake zitakurejea na kukumbuka kwann hukusema NO katika nyakati za awali...

Kuna wakati unakuwa katika mahusiano ambayo sio productive na hayana mwelekeo kabisa lakini unaamua kwendelea nayo kwa kuhofia kuonekana na watu unavunja uhusiano au kumuonea huruma yule ambaye uko nae.. 
Tambua mwisho wa siku anayepoteza ni wewe pia unaepoteza Muda katika mambo mengine ni wakati wa KUSEMA hili HAPANA (NO) endelea katika jambo kingine

Lamsingi: 
NO yako na iwe NO kiukweli isiyo na mawaa yaani isiyo ya kigeugeu ndipo utaona matokeo... katika maeneo ya ajira kuna mambo ya kusema NO katika maeneo ya Familia pia yapo katika kila nyanja... 

Uamue tu kuona lipi halina faida katika maisha yako ambalo linakukwamisha wewe kusonga mbele... 

●Je ni matumizi mabovu ya pesa SEMA NO

●Je ni matumizi mabovu ya muda jifunze kusema NO 

●Je ni matumizi mabaya ya mahusiano na watu wanaokuzunguka pia jifunze kusema NO... 

Mwanzo wa kufanya hilo/kusema NO utaona kama unaumia au unamkwaza mtu ila mwisho wa safari utakuwa umejifunza jambo jema na unefanya maamuzi mengi sahihi

Usikubali kwenda ukiwa na majibu yote mawili katika maisha yako... 

Huwezi sema ngoja nipoteze muda na hili ninachofanya au kwa huyu mtu niliye nae ili akija yule namtaka au kikija kile nakitaka basi nitakiacha hiki/nitamuacha huyu niendelee nakile nataka...

sema NO to unproductive things... 

Kwa afya ya maisha yako neno NO ni muhimu sana.... 

Usiridhishe watu au jamii kwa kuogopa kusema NO... 

NI HERI USEME NO na umuumize mtu kwa muda kuliko kisema YES umridhishe mtu kwa muda na wewe uumie kwa maisha yako yote....

Nikutakie wakati mwema... unapoenda kuanza kuyaondoa mambo yote uliyosema YES wakati jibu lako la ndani ni NO... 

Uwe na wakati mwema....
________________________________________________

Author: JOSEPH GEOTHAM MREMA
C.E.O and Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc

Visit Us
Facebook: Joseph Geotham Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Tweeter: Joseph G. Mrema
Facebook Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com

Contacts Us:
Whatsapp &Calls: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...