EPUKA KUWA MTU WA KAWAIDA

Nakusalimu Mpambanaji...

Habari za mapambano ndugu Mwanaharakati mwenzangu... 

Ni muda na wakati mwingine tena ambao tena tunakuletea moja ya mwendelezo wa makala fupi za kukukumbusha au kukutia moyo pale ambapo unaona huwezi kusogea mbele katika harakati za mafanikio na harakati za mapambano kufikia malengo yako

Katika maisha yetu tuna ndoto/maono ya kufika mahali fulani.... 

Lakini ndoto hizi zinachangamoto nyingi sana ambazo zinatofautiana kwa kila mmoja kulingana na uwezo wa akili, umri, elimu, kipato nakadhalika....

Mbali na changamoto hizo lakini bado wapo waliofanikiwa kufikia ndoto zao ambazo walizifanyia kazi na waliziatamia kwa kitambo na sasa tunawaona wakiwa watu muhimu katika dunia hii na waliosonga mbele sana kimaendeleo.

Wapo ambao wamezaliwa ni walemavu ma wengine hawana baadhi ya viungo lakini wamepiga hatua kubwa sana kwa kufanya mambo makubwa kabisa lakini wewe uko mzima kabisa kabisa na kila kitu unacho, wapo waliozaliwa katika familia za kimaskini kabisa lakini wamefanikiwa kufikia malengo yao, wapo ambao hakusoma kabisa lakini wamefikia malengo yao, wapo waliotengwa/kufiwa na wazazi lakini wamefikia malengo yao na kuishangaza dunia, wako ambao hawakuwa na vipaji lakini wamefanya maajabu...

Nini nataka kukwambia muda huu.... usidharau namna ulivyoo, usichoke namna ulivyooo, usikate tamaa namna ulivyooo.....

Tafuta eneo upambane na wewe uache alama katika dunia hii....

Usikubali kuwa wa mtu wa kawaida, usikubali kufanya mambo ya kawaida kila siku, usiridhike na nafasi uliyopo, usiridhike na kipato ukicho nacho na chanzo kimoja cha fedha, usiridhike na mali unazomiliki....

USIRIDHIKE

USIRIDHIKE

USIRIDHIKE....

Utakapoamua kutokuridhika na kuanza kupiga hatua moja zaidi ndipo utakapo badilisha mfumo mzima wa maisha yako....

Hujawahi ona mtu anamiaka 60 na bado anapambana na kitabu?? Anatafuta kutokuwa wa kawaida, hujawahi Muona mtu anamajumba na maghorofa na bado anatafuta maghorofa mengine??? Hujawahi ona mtu anahela za kutosha bank kumlisha hata miaka 100 bila kufanya kazi yoyote lakini bado anatafuta hela nyingine???? Hujawahi ona mtu ana mashamba makubwa na bado anataka mengine??? Hujawahi muona mwanafunzi ni wakwanza darasani toka anaanza la kwanza na bado anasoma kwa nguvu kuliko hata yule aliye wa mwisho???? Hujawahi kumwona mchezaji ambaye anakila kitu anajituma katika mazoezi kuliko hata yule ambaye hana chochotee????

Hawa wote wanatafuta kutokuwa wa KAWAIDA....



Wewe ni eneo lipi umelifanya kuwa la kawaida??? JE NI KAZI?? JE NI BIASHARA??? JE NI SHULE?? JE NI KATIKA KIPAJI ulicho nacho????

Badilika sasa USIWE WA KAWAIDA.... ongeza speed....

Usingoje VITU VITOKEE wewe ANZA KUVIUNDA SASA na havitakuwa vya kawaida kabisa....

Japo si kila siku mambo yatakuwa sawia lakini BIDII yako itakufanya wa TOFAUTI KABISA na ITAKUJENGEA HESHIMA POPOTE PALE..... 


ANZA KUISHI MAISHA AMBAYO SI YA KAWAIDA.... pangilia Muda wako, JIFUNZE KILA MARA, Ambatana na waliosonga mbele ili wakuongezee kiu ya kusonga mbele na kutoka eneo hili la kuwa mtu wa kawaida..... 

Maana kuna wengine wakipata tenda mahali ya kumuingizia 10,000 kila siku basi hajiongezi kutafuta tenda ya 100,000, wala hata pale alipo haboreshi ili hata thamani yake ipande anaridhika...

Kwa namna hii NDOTO YAKO NI LAZIMA IFE TU... hakuna namna... 

Uwe na wakati mwema na karibu tena siku nyingine katika makala zetu....

AMEN
_________________________________________________

Author: JOSEPH GEOTHAM MREMA
Founder of Josel Company
JOCHE INSPIRATIONAL AND MOTIVATIONAL INC

Visit Us:

Facebook: Joseph Geotham Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Tweeter: Joseph Geotham Mrema
 Fb Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com

Contacts Us

Whatsapp& Calls: + 255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...