FANYIKA SABABU YA MAFANIKIO YA MWINGINE

 Ni muda mwingine najongea kuendelea kukupatia mfululizo wa makala zetu katika Blog ya www.jocheinc.blogspot.com. Ambapo tunaendelea kutoa elimu elekezi za maisha ya kila siku...

  Nianze kwa kusema kuwa kila binadamu anajambo lake ambalo anatamani alifanye... liwe dogo ama kubwa haijalishi lakini kwa mtazamo wake ni jambo kubwa na anataka kulifanya lifanikiwe..  

 Na katika hali hiyo hutamani sana kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki katika maono yao... 

  Mtu mmoja anayeaminika ni tajiri namba moja katika Nchi ya China anaitwa Jack Ma ambaye ndie mmiliki wa Mtandao wa ALIBABA anasimulia kuwa alipokuwa na MAONO ya kuwa na ONLINE MARKET aliwaita marafiki zake

  Alipowaita marafiki zake akawashirikisha ndoto zake na maono yake ya kufanya jambo kama hilo. Anasema (Jack Ma) kuwa kipindi hicho pia hata internet ilikuwa chini sana katika Nchi ya China.. hivyo Marafiki zake hao aliowaita nyumbani kwao walimpinga na kuona na kumwambia ni jambo lisilowezekana na lakijinga aachane nalo..

  Lakini palikuwa na rafiki yake mmoja kati ya aliowaita alimsapoti kwa kumwambia jaribu unaweza ukafanikiwa... 

 Basi Jack akachukua uamuzi wa kufanya jambo hilo.. ambalo mpaka sasa limekuwa na linaendelea kukua na kumuingizia kipato kikubwa sana...

  Hii ni story fupi sana ya Jack Ma.. 

  Swali: Je wewe ni watu wangapi umewakatisha tamaa katika ndoto zao?? Au umewatia moyo katika maono yao???


  Je wewe ni muua ndoto za watu??/Muua maono ya watu?? Au mpeperusha shauku za watu za kufanikiwa???....

   Badilika sasa..  kuwa na mtazamo chanya juu ya ndoto za wenzio, Sapoti kile wanafanya ikiwezekana kuwa sababu ya mafanikio ya ndoto zao maana kufanikiwa kwao ndio kufanikiwa kwako.... 

 Fanyika kuwa sababu ya mafanikio ya mwenzio....

  Maana ni wengi ambao wako tayari kuona ndoto za watu zinakufa kuliko kuona ndoto hizo zinafanikiwa......

Badikisha mtazamo... 

 Fanyika kuwa sababu ya mafanikio ya mwenzio....

 USIWE DREAM KILLER, VISION KILLER or PASSION KILLER ukakwamisha mafanikio ya wale watu muhimu katika maisha yako...

Nikutakie wakati mwema sana... tukutane tena kipindi kijacho... 

Amen
_________________________________________________

Author: JOSEPH GEOTHAM MREMA
C.E.O and Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc

Visit Us:
 Facebook: Joseph Geotham Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Tweeter: Joseph G. Mrema
Facebook Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com

Contact Us;
Whatsapp & Calls: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...