MAISHA NI SAFARI NA UKWELI UTAKUPELEKA NJIA SALAMA
Habari za muda huu???
Nakusalimu ndugu/jamaa/rafiki/ Mwanaharakati ambaye anakimbizana kuelekea kwa kilele cha mafanikio yake....
Maisha ni safari ambayo kama zilivyo nyingine ambazo tunasafiri katika maisha yetu...
Na safari hizi kila mtu ana njia yake, wapo ambao safari yao nauli ni 400 na hufika baada ya dakika 60 yaani lisaa lizima lakini wapo ambao safari zao nauli ni 200,000 na hufika baada ya NUSU saa tuu...
Hizi zote ni safari na zote zina nauli na zote zinaelekea katika eneo ambalo wasafiri wamepanga.....
Nini nataka kusema....
Safari ya maisha yako usikopi ya mwengine maana hujui anapokwenda hujui anapitia changamoto zipi... hujui gharama gani ameingia mpaka kufikia ulipo... tafuta safari yako na mahali kule unaenda.... unaweza omba ushauri kwa mwengine lakini angalia usikopi maisha yake...
Katika Safari yako penda sana na waheshimu watu wanaokuambia ukweli....
Hawa naokuambia ukweli watakusaidia kukurejesha katika njia yako watakusaidia usiingie machakani....
Naomba utofautishe WANAOKUAMBIA UKWELI na WANAOSEMA CHOCHOTE.....
Nini namaanisha...
Si kila jambo unaloambiwa ukalikubali... lichuje lipime liangalie, je nikifuata huu ukweli ninaoambiwa faida yake ni ipi, hasara yake ni ipi???...
Mfano: Wewe unataka kuja kuwa muimbaji..
Mtu/rafiki/Ndugu anakuja anakuambia acha kuimba sauti yako mbaya...
Ni kweli sauti yako mbaya.. lakini zipo njia za kuiboresha zipo njia za kuhakikisha unafanya ili sauti yako iwe nzuri.. Hivyo wazo hilo la kuacha kuimba achana nao wewe ongeza juhudi katika kuiboresha sauti yako.....
Kwa upande wa wale waopenda kusema ukweli:
Kwanza nikupongeze kwa kupenda kuwaambia watu ukweli , lakini angalia usije ukawa muua ndoto za watu kwa kuongeza ushauri mbovu juu ya wale unaowaambia ukweli...
Ukweli ni mtamu ukimwambia mtu lakini ni mchungu ukiambiwa...
Tafuta namna nzuri ya kumsaidia na kumtia moyo yule unayemwambia ukweli wa jambo linalomuhusu...
Usije ukawa unasema ukweli kwa faida zako binafsi na kwa nia ya kujinufaisha au kwa nia ya kumkomesha mtu husika..
Ukifanya hivyo utakuwa ni mmoja ya wanaosema chochote au muua ndoto za watu....
Mwanafalsafa mmoja anaitwa Roy Bennett alisema "I respect those who tells me the truth no matter how hard it is"
Hapa aliwagusa wale wanaoambiwa ukweli... Waheshimu sana wale wanaowambia ukweli haijalishi ni mgumu kiasi gani...
Hivyo kwa muda huu nikuache na jambo hilo..
Jipime uko upande upi?? Na fanya marekebisho mahali unapokosea ili usonge mbele usibaki ulipo...
Wewe ndio dereva wa maisha yako, na anayekwambia ukweli wa mahali umekosea anapenda mafanikio yako ili safari yako isiwe na vikwazo vingi...
AMEN
_________________________________________________
Author: JOSEPH GEOTHAM MREMA
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc (JIMI)
Visit Us:
Facebook: Joseph Geotham Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Tweeter: Joseph Geotham Mrema
Blog: www.jocheinc.blogspot.com
FB PAGE: Joche Talks
Contact Us:
Whatsapp&Calls: + 255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com
No comments
Post a Comment