HOFU NA MAFANIKIO
Napenda kuwasalimu nyote na kuwapongeza kwa shughuli za siku nzima ya leo kwa kutafuta na harakati za kufanikisha malengo yako yaweze kufanikiwa kwa namna na kadri ile imeipanga iwe.
Pamoja na hayo ni muda mwingine napenda kutumia nafasi hii na wakati kukutia moyo na kukumbusha kuwa harakati uzifanyazo ni muhimu kwa malengo yako.
Haijalishi umesogeza kwa kiasi gani au umekwama kwa kiasi gani.
Maisha ni mapambano ambayo yanahitaji mtu kujitoa kwa kujikubali na kutojionea huruma kwa mlengo wa akili yake, fedha zake, muda wake na hata mali nyingine zifananazo na hizo.
Kukata tamaa ni alama ya kushindwa kupambana. Na ni mwiko askari aingiaye vitani kuanza kutazama nyuma na kujihoji hoji. Ukianza kujihoji ni rahisi kutoka nje ya lengo lile ambalo unataka.
“Ni bora upambane kwa jambo fulani kuliko kuishi bila kitu”.
Ni mstari mwepesi lakini ujumbe wake ni mzito sana. Kutopambana maana yake hujui unapoenda, hujui nini unataka, hujui unataka kuwa mtu wa aina gani, yaani kwa kifupi ni huna mwelekeo.
Usikubali kuishi bila kuwa na lengo/ndoto ya wapi unaenda, hakikisha unachora ramani ya maisha yako ya wapi unaenda na wapi unataka kufikia na wapi unahitaji msaada na wapi ukiwa mwenyewe unaweza.
“Ili ufanikiwe hamu yako ya kufanikiwa ni lazima iwe kubwa sana kuliko hofu yako ya kufeli”.
Ni kweli sisi vijana huwa tunakuwa na hofu ya kujaribu kufanya mambo makubwa.
Tunakuwa na hofu ya kufanya mambo mapya
Tunakuwa na hofu ya kujifunza mambo makubwa na mageni
Tunakuwa na hofu ya kuuliza maswali yanayotusumbua katika maisha yetu.
Lakini kwa kufanya kuikubali hofu kututawala maana yake tunakubali kutokupigania yake mambo tunayataka katika maisha yetu.
Wewe unataka kuwa mfanyabiashara pambana katika eneo lako, tafuta wale waliofanikiwa katika biashara wakutoe hofu inayokusumbua.
Wewe unakipaji cha sanaa kaa na walioweza kunufaika na vipaji vyao wakutoe hofu...
Na mengine yote yafananayo na hayo. Toa hofu fanikisha adhima yako ambayo unakiu nayo.
Nikutakiwe wakati mwema.
_________________________________________________________________________
Joseph Geotham Mrema
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc
Follow us on
Facebook: Joseph Geotham Mrema
Istagram: joseph_geotham_mrema
Tweeter: Joseph Geotham Mrema
Facebook Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com
Contact Us
Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp & Calls: +255 712 851 687
No comments
Post a Comment