MAMBO YA KUZINGATIA 2018-2

Habari ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu katika blogu na application yako ya JOCHE ambayo inapatikana katika PLAY STORE sa ANDROID.

Napenda kukuletea sehemu ya pili katika mambo ya kuzingatia katika Mwaka 2018 ambao wengi tumeuita ni mwaka wa mafanikio na kusonga mbele. Lakini pia tunapenda kuwashukuru sana nyote ambao mmetuma maoni yenu kwetu tumeyapokea na pongezi zenu pia tumezipokea. Kwa ujumla tunasema ASANTE SANA.. 

Baada ya kuona sehemu ya kwanza na kujifunza mambo machache basi karibu tuendelee katika sehemu hii ya pili na ya mwisho. Katika mwaka 2018 ndugu msomaji zingatia vitu vifuatavyo:-

  1. KUTUMIA MUDA VIZURI. Katika maisha ya mwanadamu muda ni kitu cha muhimu sana, lakini pia ni bidhaa adimu sana kupatikana na ikikupita huwa hairudi tena. Lakini pia hakuna mahali wanauza muda. Hivyo ni muhimu sana kuutumia muda wako vyema, hasa katika mambo yenye faida. Mafanikio yako yamefungwa katika muda. Na kila kipindi kina hatua unatakiwa uwe unafanya ili uweze kufanikiwa kwa viwango. Lakini  jamii ya watu wengi wameona kupoteza muda ni jambo la kawaida. Ni rahisi kusikia mtu anakumbia nipo hapa napoteza muda, au namtafuta fulani tukapoteze muda, hili sio jambo sahihi na halitasababisha mafanikio katika maisha yako. Jifunze kupanga ratiba zako vyema. Jifunze kufanya kila jambo kulingana na ratiba hasa yale yanayochangia katika mafanikio yako. Hivyo katika 2018 tunakukumbusha kuwa MUDA BIDHAA ADIMU hivyo itumie vyema kwa manufaa ya mafanikio yako
  2. MTANDAO WA MARAFIKI FAIDA. Ni muhimu kujiuliza nani ni rafiki yako wa karibu, au rafiki zako ni akina nani? Wanamchango gani katika maisha yako na hasa juu ya kufikia malengo yako ukiyojiwekea katika 2018? Au kila mtu akija wewe unabeba tu? Pasipo kuangalia faida na hasara za hiyo rafiki? Ni muhimu kutambua aina ya rafiki wanaokuzunguka ili uweze kujua namna ya kukaa nao na kuzungumza nao. Maana marafiki wanamchango mkubwa sana katika mafanikio yako hasa zile harakati za mapambano. Kama marafiki zako ni wapambanaji nasi na wewe utakuwa tu kama wao lakini ukiwapata marafiki wavivu hawatakushauri juu ya ufanyaji kazi. Hivyo jitahidi uzungukwe na marafiki wanaokuhamasisha kufanya mambo yanayoleta mafanikio au yanayosababisha mafanikio katika maisha yako. 2018 chagua rafiki sahihi kwa jambo sahihi.
  3. ANZA NA ULICHONACHO. Katika maisha ya mwanadamu hakuna wakati sahihi wa kufanya jambo. Kila wakati ni sahihi wa kufanya mabadiliko, wa kuwekeza, wa kuonyesha mapambano halisi ya mafanikio. Kubali kuanza kwa udogo maana kukua kwa kile kidogo ndio mafanikio yenyewe tunayasema. Watu wengi hasa vijana wameogopa kuanza na kile walichonacho na hii imewafanya kuendelee kupoteza muda. Anza kuonyesha nia ya jambo unalotaka mtaji utakukuta njiani au utaukuza wakai unaendelea mbele katika mafanikio yako. Wekeza hata kama ni shilingi Elfu Hamsini (50,000/-). Kwa kuwekeza huko patafungua mlango mwingine wa vyanzo vya mapato.
  4. EPUKA HOFU. Hisia za kuona unashindwa au unaona huwezi ndio tunazozizungumzia hapa. Kuna hofu nzuri na hofu ambayo inakugharimu katika maisha yako. Ni kweli umepanga mipango inahitaji fedha nyingi au inahitaji akili nyingi sana lakini ukiweza kuishinda hofu ndipo mafanikio ya malengo yako yanapokuja. Hata vitabu vya dini mbalimbali vimekazia sana juu ya kutoogopa katika maisha yako, kuepuka hofu na fikra za kukufanya ushindwe kujiamini katika mambo mbalimbali. Wapo waliotangulia kufanikiwa wasikutishe kuwa wewe hutaweza, lakini jambo ambalo ni baya ni pale unapokatishwa tamaa na watu kwa kuwaangalia waliofeli katika jambo unaloliendea. Usitishwe nao hao walioshindwa. Ila hakikisha ujifunza kwa waliofanikiwa na kusonga mbele. Hapo utakuwa umeshinda jambo muhimu sana kuelekea katika mafanikio yako.
  5. ZINGATIA IBADA. Wengi wetu tunaamini sana juu ya kufanikiwa pale unapoombea au kufanyia dua vile vitu tunavyovifanya. Lakini pia pasipo kujali ni dini gani unayoamini ni muhimu sana kuzingatia ibada na kumuomba Mungu/au kile wewe naamini ili kuweza kufanikiwa. Zamani walikuwepo wazee ambao walioamini sana juu ua miungu mbalimbali kuwa inawaletea mafanikio katika maisha yao. Vivyo hivyo hata wewe pia ni muamini wa Imani fulani basi zingatia IBADA, ombea mipango yako, ombea njia zako ili uweze kufanikiwa, kama ni Mkristo najua unajua ni nini unatakiwa ufanye, kama ni Muislamu pia najtambua unajua nini kinapaswa kufanya, halikadhalika na Hindu, Wapagani na kadhalika. IBADA ni jambo la Muhimu katika kufanikisha mambo yako hivyo usiache kufanya kila wakati na kila mara katika mwaka 2018.
MWISHO: Kila mtu ananamna yake ya kupambana ili afanikiwe, usiogopeshwe na njia za mwenzio, wala kukata tamaa. Weka juhudi katika mikakati yako. Ongeza nguvu na maarifa zaidi pale unapoona ugumu, usisite kuomba msaada pindi unapoona ugumu au unakosa dira. Zaidi ya yote nikushukuru sana kwa kujiunga nasi katika makala hii na kujifunza vitu kadhaa wa kadhaa. 

Usiache kututukia maoni yako kwa namna na email iliyopo hapo chini, kwa kututumia Ujumbe mfupi au kupiga kabisa.

Lakini pia tunapenda kukumbusha juu ya  kudownload application yetu katika playstore yako. Inaitwa JOCHE.

Asante
Joche
_____________________________________________________
Author: Joseph Geotham Mrema
Blog: www.jocheinc.blogspot.com

Application : JOCHE

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...