MUDA NA NDOTO

Hello? Habari ya wakati huu? Karibu tena katika mfululizo wa makala zetu za kuhamasisha na kufundisha kwa jamii yote na watu wote wa rika zote. 

Kila siku huwa na masaa 24 ambapo kila mtu aliye hai huwa na masaa hayo ambayo hukamilisha siku nzima iliyo na masaa 12 mchana na Masaa 12 usiku.

Katika masaa hayo wapo watu ambao hufanya malengo yao kuendelea kusonga mbele na kuzailisha zaidi lakini pia kuwekeza zaidi na wapo ambao hudumaa yaani hawa hawasongi mbele wanabaki hapo walipo kila siku hawasogei mbele maana hawajawekea juhudi katika malengo yao. 

Kwa kuweza kutumia muda vyema basi kuna kupelekea katika kufanikisha malengo yako na ndoto zako za kuwa mtu wa aina gani hapo mbeleni. Usipojifunza kutumia muda wako vyema ni vigumu kuyafikia kwa wakati muafaka.

Only dreams zinakufanya uwe hivyo ulivyo... kama your dreams hazikufanyi ukawa na njaa ukawa na uhitaji ukaweza kusacrifice vitu unavyovipenda bado hizo ndoto zako sio za kiwango chako.

Ndoto ambazo hata ukiziangalia zinakutisha ukimsimulia mtu anaogopa hizo ndio zitakazokufanya uende mbio na hata muda mwingine kukosa usingizi.

Muda mwingine kujinyima kwenda maeneo fulani, muda mwingine kutokuwa na watu fulani ili kuona jambo lako linatimia...

Safari ya kufikia ndoto zako ni kama safari ya kwenda mbinguni (😊

Kuna kujikana kuna kujibana kuna kujitesa kuna kujitoa kuna kujigharamia kuna kila aina ya changamoto lakini lengo ni uone unafanikisha safari ya kufika Uzimani.

Ndivyo katika Ndoto tulizonazo... kuna muda unajitesa unajibana unajikinga unajizuia unakesha ili tu uone ndoto zinatimia

Ukishatambua hayo basi utaanza kupambana kwa kila eneo.


Siku zote muda hautoshi.

Kinachotakiwa ni kutengeneza muda.

Somebody says ukiona mtu anakwambia kuwa hana muda juu ya jambo fulani ujue jambo hilo sio kipaumbele kwake.

Hivyo ukiona bado jambo unaliacha kwa kuona muda huna ujue hilo jambo bado halijagusa katika moyo wako wala halina effect katika maisha yako.

Swala la Muda kila eneo ni lazima utengeneze.. katika mahusiano ukikosa muda na mwenzio ni changamoto (mambo hayaendi na uhusiano utakufaa tu) ukikosa muda na familia ( familia itavurugika tu kila mtu atafanya lake) ukikosa muda kwenye malengo yako (lazima ukwame tu maana utakosa muda wa kuyaassess na kuexamine wapi umekwama na utengeneze wapi usonge mbele zaidi).

Hivyo MUDA HUTENGENEZWA NA MALENGO na SIO MALENGO KUTENGENEZWA NA MUDA.
_________________________________
Author: Joseph Geotham Mrema
Joche Inspirational and Motivational Inc
Contacts: +255712851687 (Whatsapp)
Dowload Our Application : JocheApp

FOLLOW US:

Instagram: joseph_geotham_mrema
Facebook: Joseph Geotham Mrema


Tweeter: Joseph Geotham Mrema

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...