KUELEKEA PALE
Maisha yanafananishwa na safari kama zilivyokuwa safari nyingine.Kila mmoja wetu anapambana hapa na pale ili aweze kufikia katika hatma yake.Katika safari yoyote ile ni lazima kuwe na dhoruba na adha za aina mbalimbali. Kwamfano, katika barabara unaweza
kukutana na milima, mabonde na makorongo. Katika maji unaweza kukutana na mchafuko hali kadhalika ukitumia usafiri wa anga unaweza kukutana na hali mbaya ya hewa.Lakini pamoja na haya yote huwa tunafanikiwa kufika katika yale maeneo tunayoelekea.Vivyo hivyo katika maisha kuna muda tunapitia changamoto kali na ngumu kiasi cha kukata tamaa...kuna changamoto za kiuchumi,kisiasa, kiroho,kijamii na nyingine nyingi. Katika hizi zote yamkini kuna watu tuliowategemea sana na wakageuka kuwa miiba. Kuna usemi mmoja wa lugha ya kiingereza unaosema,"the world is a classroom and every person you meet is a teacher "
Unapokutana na kuona watu hawapo pamoja na ww usiwalaumu wala kuwachukia. Unapaswa kutambua na kuamini kwamba ipo hivyo ilivyo kwa ajili ya kukujenga na kukufanya uwe bora zaidi. Katika kila gumu unalolipitia linakutengeneza na kukufanya uwe bora zaidi,kwani hauwezi kuimarika bila kubomoka, kutingishwa na mengine mengi yafananayo na haya.Swali la kujiuliza, Je,nifanye nini wakati ninapokuwa napitia magumu ili nisiiharibu safari yangu?Kuna mengi sana ya kufanya juu ya hili lakini kwa ujumla unapaswa kujua wewe ni nani? Unatoka wapi? Unataka nini?Unaelekea wapi?Pamoja na kuwa na tumaini, imani na uvumilivu. Ukijua unachokitaka utapambana mpaka uone mwisho wako.Pia unapaswa kujitamkia mema na ushindi kutoka ndani yako kwani tuna nguvu ya uumbaji. ...jipe moyo jiambie ni naweza, ntapambana na nitafika hata iweje.
Kuna siku utasimama na kufurahi na kusema ni kwa sababu sikukata tamaa na kuishia njiani .
Inawezekana #Jiamini
# pigania ndoto zako
# una nguvu.
#ririwords
JocheApp
________________________________________________
JocheApp
No comments
Post a Comment