NAFASI YAKO KWA WENGINE
Je,umewahi kujiuliza kuhusu Umuhimu,mchango na nafasi yako katika maisha ya wale wanaokuzunguka?
Je,umewahi kuona ,kutambua na kuthamini mchango wa watu wengine katika maisha yako?
Je,umewahi kuona ,kutambua na kuthamini mchango wa watu wengine katika maisha yako?

Kuna wakati tunakuwa na hisia za kufanya vitu mbalimbali kwa ajili ya watu wengine. Je,ni mara ngapi tunawafanyia watu yale tuliyoguswa kuwafanyia,pasipo kuangalia mapungufu yao na mambo mengine ambayo yanaweza kuwa yametukwaza kutoka kwao?Hapa duniani tumeumbwa katika hali ya kutegemeana kwa namna moja au nyingine,hivyo basi tujitahidi kuwepo kwa ajili ya wengine pasipo kuangalia sababu.Je,unajua neno lako moja linaweza kuokoa maisha ya mtu na kuyadidimiza pia?Hivyo basi tuna nguvu ndani yetu kwa ajili ya watu wengine pia.Kwa hiyo tupende, tujali na kujitoa kadri uwezavyo.Kesho haijaahidiwa.
#ririwords
JocheApp
_______________________________________________
JocheApp
No comments
Post a Comment