THAMANI NDANI YA MTU
Habari za saa ndugu msomaji. .. ni matumaini yangu unaendelea vizuri ktk mapambano ili uweze kufikia ndoto na malengo yako.
Huko Italy kulikuwa kuna jiwe moja ambalo ndani ya hilo jiwe ilitakiwa kuchongwa sanamu ya Daudi.
Kuna watu wawili ambao ni Agustino na Antonio walipewa kazi ya kuchonga sanamu hiyo..lakini walishindwa wakasema jiwe hilo haliwezi kutoa sanamu nzuri.
Baada ya miaka 25 baadae kazi hii alipewa mtu aliyeitwa Michangelo. ..baada ya miaka mitatu alikuwa ameshamaliza kuchonga na alipata sanamu nzuri tu na ilikuwa ni mwaka 1504.Sanamu hiyo ni kivutio cha watalii wengi mpaka leo hii .Mamilioni ya watalii hufika na kuitazama sanamu hii.
Siku moja papa akamuuliza umewezaje kupata sanamu ndani ya jiwe hili?
Naye akajibu, akasema nilimuona Daudi tayari ndani ya jiwe hili hivyo nilichokifanya ni kutoa kile ambacho si Daudi ili Daudi abakie na aonekane vizuri.
Kutokana na habari hii fupi kuna mengi sana ya kujifunza lakini kwa leo tuangalie kwa ufupi mawili matatu.
Yamkini kwenye maisha kuna watu ambao wanakudharau na wanakuona si kitu...hao ni kina Antonio na Agusto. kamwe usiwaruhusu wakufanye ujione wewe si kitu,huna thamani na hauwezi kwani ndani yetu kila mtu amewekewa kitu cha thamani sana na Mungu kwa ajili ya kutimiza kusudi lake hapa duniani.
Lakini pia kuna watu ambao ni Michangelo ktk Maisha yako. ..kuna watu wanaona vitu vikubwa ndani yako,kuna watu ambao wanapambana sana kuwa karibu yako ili waondoe vile ambavyo sio wewe ili ubakie wewe.Yamkini watu hawa wameletwa na Mungu kwenye maisha yako, Je,ni mara ngapi umewafukuza, umewatusi, umewadharau na kuwaumiza akina Michangelo? Pengine ni katika huduma,mahusiano elimu na mambo mengine?
Na ni mara ngapi umechukua jukumu la kuwa Michangelo wako mwenyewe?ukaangalia yale mambo yote mabaya yanayokufanya usiwe halisi?
Chukua hatua sasa.
Tafakari
Jiulize
Sikiliza hizo sauti.
#ririwords
#theroadtothere
JocheApp
________________________________________________
JocheApp
No comments
Post a Comment