INJINI 11 ZA KUJA NA MAWAZO MAZURI YA BIASHARA - 1
Wazo zuri la biashara ni Mali yako kama ukilfanyia kazi. Kama hutalifanyia kazi ni Mali ya watu wengine. Karibu katika katika introduction ya Kozi fupi inayoitwa , INJINI 11 ZA KUJA NA MAWAZO MAZURI YA BIASHARA. KOZI HII ITAKUWEZESHA UJUE SIRI NZITO YA NAMNA NILIVYOWEZA KUJA NA FURSA 101, UKIELEWA KOZI HII UNAWEZA KUJA NA WAZO ZURI HATA ZAIDI YA MAWAZO NDANI YA FURSA 101 KULINGANA NA MAZINGIRA YAKO.
MAKAMPUNI MAKUBWA DUNIANI YALIANZA NA WAZO ZURI.
WAZO ZURI NI KAMA MBEGU INAYO OTA, INAKUA NA KUWA MTI MREFU MKUBWA.
MAKAMPUNI MAKUBWA KUANZIA APPLE MPAKA GOOGLE.
EXXON MPAKA COCA COLA
ALIBABA MPAKA AMAZON
IPP MPAKA AZAM
EFM MPAKA CLOUDS MEDIA
MO ENTERPRISES MPAKA DANGOTE
MAKAMPUNI HAYA YOTE YALIANZA KAMA WAZO KUTOKA KWENYE KICHWA CHA MTU AMBACHO HATA WEWE UNACHO.
LAKINI LAZIMA UENDE ZAIDI YA WAZO ZURI KUJENGA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.
Ingawa kwa kuanzia lazima uwe na wazo zuri ili uwe na nafasi nzuri ya kufanikiwa kibiashara.
Njia rahisi ya kufeli kibiashara ni kuanza na wazo la ovyo.
Wazo baya linaweza kukugharimu muda na pesa.
Wazo baya linaweza kukuharibia mahusiano yako na watu ambao wamewekeza kwako.
Kila mwaka kuna watu wanaacha kazi na kuingia kwenye biashara na wazo la biashara baya. Na kupoteza kila kitu.
Kuna wastaafu ambao wengine wamewekeza pesa kwenye wazo baya la biashara, wakapoteza pensheni zao. Wazo linaweza likawa zuri kwenye akili yako lakini likawa baya kwenye soko lako.
Kuna watu ambao walifilisika kwasababu walianza na wazo baya.
Kama hutaki kupoteza pesa zako, kufilisika na kuishia kuwa masikini pamoja na kwamba una nia kubwa ya kufanikiwa kibiashara basi hakikisha unanifuatilia vizuri kwenye kozi hii ambayo ni utangulizi tu.
Kama unatafuta wazo zuri la biashara ambayo ndiyo fursa yako,
Au kama tayari una wazo zuri la biashara utangulizi wa kozi hii utakufanya ujue kama upo njia sahihi.
Kabla sijaenda kukuonyesha namna ya kuja na wazo zuri la biashara, hebu kwanza tujue wazo zuri la biashara ni nini?
Wazo zuri la biashara ni lile wazo lenye sifa zifuatazo:
1. Wazo zuri ni lile linalozalisha pesa.
Kuwa na wazo kubwa ambalo hujui utaingizaje hela siyo biashara. Hata kama wazo lako ni passion yako, au hobby yako kama hakuna namna ya kuingiza hela hakuna wazo hapo. Wazo linaweza kuonekana kubwa. Wazo linaweza kukufanya ujisikie raha. Wazo linaweza kukufanya uonekane una akili sana lakini kama halitaingiza hela ni sawa sawa na bure. Halina maana. Wazo lako lazima likubaliane na soko, kwamba linaweza kuleta pesa. Wazo ambalo halikubaliki sokoni halina maana hata kama wewe unaliona ni kubwa.
2. Wazo zuri ni lile ambalo linaendana na wewe.
Yaani linaendana na mazingira uliyopo. Linakubalika na soko unalolenga. Linaweza kulipiwa na soko husika. Una ujuzi na vifaa vya kulitendea kazi. Una watu na koneksheni wa kukuwezesha au kulifanyia kazi. Kuwa na wazo kubwa bila ujuzi wa kulifanyia kazi , bila koneksheni ya watu wa kukusaidia kulitendea kazi ni ubabaishaji tu. Unahitaji watu wenye ujuzi ambao huna kusaidia wazo lako lifanye kazi, unahitaji watu wenye vitu ambavyo huna, unahitaji watu wenye pesa ambazo wewe huna ili wazo lako litembee bila hivyo wazo lako hata liwe zuri vipi ni sawa sawa na bure.
3. Wazo zuri ni lile ambalo una uhakika nalo na unajiamini nalo. Kama wazo lako halikuhamasishi, halikusukumi kuchukua hatua kubwa na hata kutake risk basi hilo wazo ni ubabaishaji tu. Wazo la kujenga Microsoft , lilikuwa na nguvu kiasi ambacho lilimsukuma Billgate kuacha Chuo ili alifanyie kazi. Wewe wazo lako lina nguvu kiasi gani ndani yako? Wazo la kujenga Facebook lilimsukuma Marke Zuckerberg akadrop out kutoka shule. Wewe wazo lako likoje? Wazo langu la kuanzisha Smart Village Agri hubs limenifanya nihamie kijijini pamoja na kwamba nimeishi na kukulia maisha yangu yote mjini Dsm. Kuna watu wanarisk kufanya vitu kama vichaa kwasababu ya nguvu ya wazo linalowaendesha. Kama hujisikii nguvu na imani kubwa juu ya wazo lako , kama huwezi kurisk kupoteza chochote kwaajili ya kulifanyia kazi wazo lako maana yake wazo lako halina sifa na si la kwako.
Hivyo basi hizi ni sifa kuu za wazo zuri , ambalo ndiyo fursa yako. Fursa zote 101 utakazozipitia kama fursa hiyo haina hizo sifa tatu basi , siyo fursa yako wala siyo wazo zuri kwako.
WAZO ZURI LAZIMA LIINGIZE HELA.
WAZO ZURI LAZIMA LIENDANE NA WEWE.
WAZO ZURI NI LILE AMBALO UNA UHAKIKA NALO NA UNAJIAMINI NALO.
Katika kozi hii ya Utangulizi, nitakuonyesha njia 11 za kuzalisha wazo zuri la biashara, na njia za kuyafanyia kazi. Hizi njia zinaitwa INJINI 11 za kuja na wazo zuri la biashara zilizosababisha kuzaliwa kwa fursa 101.
Utajifunza mifano halisi ya watu waliofanikiwa kutumia njia hizi kuja na wazo zuri la biashara,
Nikiwa namalizia utangulizi huu ambao ndiyo utakaotupeleka mpaka kwenye injini 11 za kuzalisha wazo zuri la biashara, naomba kwanza nikuonyeshe safari kubwa ya wazo la biashara na njia ambazo lazima wazo hilo lipite:
1. KUBUNI WAZO LA BIASHARA.
Hapa ni pale ambapo, unakuja na wazo zuri, unaumiza kichwa na kubuni wazo zuri , hapa ni pale unapoanza kuwa na NDOTO. Watu wote tumepitia hapa. Hapa unaweza kuwa na mawazo mengi sana lakini lazima uingie hatua ya pili.
2. CHAGUA WAZO LAKO BORA.
Hapa ni kuchagua wazo bora linalokugusa lakini linalogusa zaidi soko lako. Linakubalika na soko lako.
3. UHAKIKI WA WAZO LAKO KWA KITALAAMU IDEA VALIDATION.
Hii ni hatua muhimu sana, ambapo lazima ufanye maamuzi ya kulihakiki wazo lako. Kivipi? Lazima utafute wateja wachache wa majaribio, wakikulipa pesa kwa wazo hilo basi hapo umeli validate. Kama hakuna mtu yeyote aliye tayari kukulipa pesa, wazo lako linahitaji kuangaliwa upya. Tutakuja kusoma kiundani kuhusu hilo mbeleni kwenye kozi hii. Kumbuka kwamba , kabla hujaingia na kuanza rasmi biashara kulingana na wazo lako lazima ulihakiki wazo lako kwa watu wachache wa karibu uone , ili usipoteze pesa nyingi kama ikitokea kwamba wazo lako halikubaliki na soko
4. ANZA
Hapa ni pale ambapo unaingia rasmi kwenye biashara, baada ya kuhakiki wazo lako kwa wateja wachache sasa unaingia kwa kuwafuata wateja wengine wengi kulingana na kianzio chako. Hapa ni muhimu sana ukumbuke, wazo lililo kichwani halina maana kama hujachukua hatua yoyote.
...................Inaendelea...................
Mwandishi
Fursa 101
No comments
Post a Comment