FANYA SASA HIVI/ DO IT NOW

Imeandikwa na Joche na kuletwa kwako na JocheApp

Hello
Habari ndugu mfuatiliaji wa makala zetu katika blog yetu ya www.jochein.blogspot.com au katika Application yetu ambayo inapatikana katika PLAYSTORE ya vifaa vya Android ijulikanayo kwa jina la JocheApp.

Maisha ni safari, na ni safari yenye milima na mabonde, pasipokujali unaelekea wapi. Ni rahisi sana mwenye safari kuchagua anapokwenda au kupanga wapi anataka kwenda. Hivyo basi katika kupanga huko kunapaswa kuwepo kwa kuchukua hatua ili iweze kufanikisha safari hiyo. Safari haianzi tu ghafla lazima utapaswa kupanga wapi unaenda, nini utafanya ufanye huko unapokwenda na nini ubebe katika safari yako lakini pia mwisho wa safari yako nini unataka kufanikisha (malengo) Nimetumia lugha ya picha ili tuweze kuelewana mapema.

Hivyo basi jamii yetu ya kiafrica ni rahisi sana kupanga ni rahisi sana kufikiria vitu lakini katika utekelezaji wa kile tumepanga ni kugumu sana. Visingizio vimekuwa ni vingi lakini wengi wetu ni HOFU huwa inatusukuma kurudi nyuma. Hofu ya kushindwa, Hofu ya hasara, hofu ya jamii itanionaje? PIA kuna kitu kingine kinaitwa FIKRA POTOFU/HASI. Wengi wetu fikra potofu au hasi zimekuwa zikitutafuna ndani kwa ndani. Tunaogopa kufanya baadhi ya mambo kwa sababu tunaona ni vitu vya watu wa daraja fulani au watu wa jinsia fulani ili hali hivyo vitu ukifanya havina madhara wala havikupunguzii chochote pindi unapoanza kuvifanya au kuwekeza katika hayo maeneo.

Kwa upande wa Vijana ambao ndio nguvu ya Taifa lakini pia ndio watu wanaotazamiwa kuleta mabadiliko makubwa katika maeneo kadha wa kadha mambo haya mawili yamekuwa yakitukwamisha kusonga mbele. Yametukwamisha kufanya mabadiliko chanya katika maisha yetu lakini pia katika jamii inayotuzunguka

Jambo la Msingi ninalokushauri ni KUANZA SASA KUFANYA au KUKIISHI CHOCHOTE kile unataka au umepanga kitokee katika maisha yako.

Mfano:
♻️Je unataka kuwa mfanyabiashara? 
Anza sasa kufanya biashara hiyo, kwa kiwango ukichonacho usiogope. Haijalishi ni kiwango gani unacho. Kama ukishindwa kutumia kiwango kidogo kupanga kufanya aina ya biashara ni vigumu kupanga na kufanya maamuzi sahihi ukiwa na kiwango kikubwa cha fedha.

♻️Unataka kuwa mfanyakazi bora? 
Anza sasa kujifunza mbinu za kuwa mfanyakazi bora, kusanya maarifa yanayohusiana na eneo hilo. Pasipo kuangalia chochote au kuhofia lolote. Kila jambo lipo ndani ya uwezo wako. DO IT NOW.

Unataka kutimiza malengo yako? Wakati wa kuanza ni sasa, usiangalie changamoto inayokuzunguka, usiangalie jamii inatazama nini na inawaza nini juu yako. Kiufupi watu wote waliopiga hatua kimaisha hawakuwahi kueleweka hapo awali. Walifanya mambo kwa namna ya tofauti na jamii vile imezoea na ndio maana wakawa wa tofauti hata katika kiwango cha maisha. 

Kila kitu kinawezekana kwa namna ile unataka lakini kama hutaanza sasa hivi ni ngumu kufikia unachokitaka. DO IT NOW....

DO IT NOW.

DO IT NOW.

Nikutakie wakati mwema. Unapoendelea kujipanga kuanza kuyatimiza malengo..

Lets mit at the top of our success...
JocheApp
—————————————————-
Author: Joseph G. Mrema
Contact: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com
JocheApp

—————————————————-

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...