UTOFAUTI WAKO NDIO MTAJI WAKO
Imeandikwa na Joche na kuletwa kwako na JocheApp
Hello
Habari ndugu mfuatiliaji wa makala zetu katika blog yetu ya www.jochein.blogspot.com au katika Application yetu ambayo inapatikana katika PLAYSTORE ya vifaa vya Android ijulikanayo kwa jina la JocheApp.
Kila siku katika maisha tunakutana na gunduzi mbalimbali ambazo nyingine ni bora na nyingine si bora kwa misingi ya kwamba hazileti mabadiliko chanya katika Dunia.
Pamoja na hayo yote bado tunasema ni gunduzi na zinaheshimiwa kama gunduzi nyingine.
Leo natamani kuweka mkazo sana katika eneo la umuhimu wa mtu kujitambua yeye ni nani kwa nani yuko hivyo, na si kwa vile alitamani kuwa.
Katika Dunia hii/ Ulimwengu huu kila mtu ni wa tofauti yaani hakuna anayefanana nae. Ndio maana kuna Joche au Adam au John au Halima au Monalisa au Sara au Jackie au Anna au Rachel au Joyce au Doroth mmoja tu ambaye anavitabia vya kwake na ana mitazamo ya kwake ana umbo la kwake. Hivyo vinamfanya awe wa tofauti na mwingine. (Tunaweza fanana majina lakini hatuwezi fanana kila kitu).
♻️Nini nataka kukisema mbele yako?
Pamoja na utofauti huo wa kila mtu lakini bado ni watu wachache sana ambao wamejikubali na kuamua kuishi maisha yao? Na kuambua kuwa vile walivyo?
Je unafahamu muda mwingine utofauti wako ulionao ndio mahali ambapo mafanikio yako yanaweza kuwa yamefungwa hapo?
Je unafahamu utafauti wako ndio unaufanya Dunia kuwa ya kushangaza kila siku na kufurahisha?
Je unafahamu utofauti wako ukijumlisha na wa mwingine huweza kuleta mafanikio chanya/hasi katika dunia?
Je unafahamu utofauti ulionao unakufanya kuwa mtu wa pekee kabisa katika Dunia?
🌐 SWALI LA MSINGI?
- Kwanini kutamani kuwa kama mtu mwingine?
- Kwanini kuishi maisha kama ya mwingine
Sina maana ya kudharau aina ya maisha uliyochagua ila natamani kukukumbusha kuwa DUNIA inakuhitaji wewe na utofauti wako.
Vipo vichache vya kufanya ili uvuke hilo eneo:
✍🏼1. JIKUBALI
Ni watu wachache sana ambao wanajikubali vile walivyo. Na walipojikubali na Dunia ikawakubali. Ikaona utofauti wao na wakasonga mbele. Lakini usipojikubali na kutaka kuwa kama fulani, tunakuwa tunaona picha ya yule mtu kama kivuli na unakuwa umejificha nyuma ya pazia la mtu huyo ambaye unapenda kuonge kama yeye, unatembea kama yeye, unavaa kama yeye, unafanya kila kitu kama yeye.
Hapa naweka mkazo wa JIFUNZE KUWA WEWE.
✍🏼2. USIOGOPE KUWA WA TOFAUTI KATI WA WATU WANAOKUZUNGUKA.
Ni rahisi sana kudandia aina ya maisha ya mtu fulani lakini ni vigumu kukubali aina ya maisha unayoyataka kuishi.
Usiogope kuambiwa wewe mbona unafanya mambo kiutofauti. Ni kweli unatakiwa kufanya tofauti kwa sababu wewe ni wa tofauti hupaswi kuigiza hapo.
✍🏼3. JITAMBUE
Ni vyema sana kujitambua hasa katika eneo la kipi unaweza kipi huwezi kipi Mungu kaweka ndani yako na kipi unahitaji msaada.
Binadamu tumeumbwa kwa misingi ya kusaidiana. Kuna vipaji ambavyo haviwezi kusimama vyenyewe bila sapoti ya kipaji kingine ili vyote kwa pamoja vikue na kuibadikisha Dunia.
✍🏼4. UTOFAUTI WAKO NDIO UTAMBULISHO WAKO
Ni kweli hili jambo. Unapokuwa wa tofauti tunakutambua kwa utofauti huo. Hakuna namna ya kukutambua kama sote tungekuwa na mitazamo sawa, maumbo sawa, sura zinafanana, Rangi zinafanana. Imarisha utofauti wako maana ndio utambulisho wako na ndio fahari ya dunia hii.
Kwenye Kitabu kimoja cha Dini (Biblia) kuna mstari unaosema
“Nalikufahamu kabla ya kuumbwa kwa misingi ya Dunia/Ulimwengu”
Hii inamaana Mungu amekuleta Duniani kwa makusudi maalumu kabisa.
Jikubali wewe ni wa tofauti, fanya mambo kitofauti, kila kitu kiwe tofauti na usiogope kuonekana wa tofauti.
Wewe ni Mtu wa Tofauti Kabisa.
Nikutakie wakati mwema.
Mungu akubariki na kukuimarisha uendelee kusonga mbele.
JocheApp
—————————————————-
Author: Joseph G. Mrema
Contact: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com
JocheApp
—————————————————-
No comments
Post a Comment