KWANINI KUTENDA WEMA NA HAKI?
Hello
Habari ndugu mfuatiliaji wa makala zetu katika blog yetu ya www.jochein.blogspot.com au katika Application yetu ambayo inapatikana katika PLAYSTORE ya vifaa vya Android ijulikanayo kwa jina la JocheApp.
Team nzima ya Joche tunakusalimu na kukukaribisha tena katika ujumbe huu ambao tumelenga katika kukuongezea mitazamo kadhaa ndani yako lakini pia kukuongozea nguvu ya kusonga mbele. Na hiyo ndiyo kazi yetu kuhakikisha kila usomapo makala zetu huchoki kusoma na kila ukirudia unakutana na jambo la kujifunza kila siku.
Leo tunaanza kama ifuatavyo:
Katika maisha yetu ya kila siku kuna maeneo ambayo tunayapitia ama tunaishi ama tunafanya shughuli zetu za kila siku (hapa naongea na wafanyakazi). Lakini pia kuna kundi kubwa sana la vijana ambalo ni wanafunzi pia hawa nao wanachangamoto zao ambazo kimsingi zinatofautikana au kwa namna moja au nyingine zipo zinazofanana sema kila mtu kuna namna au jinsi ambayo hutumia kutatua changamoto hizo.
Kuna changamoto ndani ya familia, kuna changamoto ambazo zipi katika eneo unaloishi na hizi zote zina maana na makusudi kuja katika maisha yako ya kila siku.
Wapo watu wanaoweza kugeuza changamoto kuwa fursa. Mfano wapo ambao katika maeneo wanayoyaishi kuna ukame wa maji safi wakatatua changamoto hizo kwa kuchimba visima, lakini pia wapo ambao wameweka matank makubwa na kujaza maji na kuuza. Hapa mtu huyu kageuza changamoto ikawa fursa.
Pamoja na hayo lakini pia kuna swala la changamoto katika uhusiano kati ya mtu na mtu (sio lazima mahusiano ya kimapenzi). Inaweza ikawa mahusiano ya kibiashara, au hata ujirani mwema. Ndani ya huo uhusiano unaweza jitoa kwa kila namna kwa kila hali lakini bado mtu wa upande wa pili wa mahusiano hayo asithamini yote mazuri uliyoyafanya lakini akabaki na lile moja tu ambalo hukulifanya.
Usichoshwe na mahusiano hayo hiyo ni tabia ya watu wengi.
Mwanafalsafa mmoja wa kimarekani aliwahi kusema ,”Unaweza kufanya mambo 99 kati ya 100 kwa mtu fulani, lakini akakumbuka jambo moja ambalo hukumfanyia”.
Nini nataka kuweka bayana:
🌐Usichoke kutenda mema hata siku moja.
Kila siku dunia inakutaka utende mema. Usipoteze thamani yako kwa kujaribu kulipiza kisasi kwa watu kwa kuwa uliwatendea wema wao hawajakutendea wema. Changamoto zipo tu kila mahali. Pambana na kuiweka taswira ya wema ndani ya moyo wako na jamii inayokuzunguka. Kuna methali moja ya zamani sana inasema ,”Tenda wema nenda zako”. Yaan baada ya kufanya yote usingojee kutendewa wema wa watu husika. Wakitenda pokea wasipotenda endelea na safari yako.
🌐Usiache kutenda haki.
Pamoja na kutenda mema kwa watu. Hakikisha haki inatendeka kwa watu wote. Usifanye wema kwa mtu huku umeminya haki ya mtu mwingine. Zamani watu walikuwa wanasema ukiwa na ndugu ambaye ana nafasi mahali fulani basi utathaminiwa sana kuliko mwingine. Unaweza kufanya hivyo lakini ujue haki ya mtu haidhulimiwi. Usitoe Rushwa/Hongo/Takrima au kupokea ili uminye haki ya mtu/ watu kwa manufaa ya watu wachache.
♻️Unaweza tumia nguvu kubwa sana kufikia kilele cha mafanikio yako kama hutazingatia mambo haya mawili. Japo ni madogo kwa mtazamo lakini ni makubwa kama usipoyathamini.
Mapambano yanaendelea. Usiku na mchana lazima tuatamie ndoto zetu. Ili tufike pale tunapotaka.
Hakuna kukata tamaa daima, ikishindikana njia moja tunachonga njia nyingine mpaka tuhakikishe tunafika pale tunapotaka.
Tunakutakia wakati mwema.
JocheApp
—————————————————-
Author: Joseph G. Mrema
Contact: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com
JocheApp
—————————————————-
No comments
Post a Comment