JIPE TUMAINI JIPYA MAANA KESHO YAKO IPO
Imeandikwa na Joche wa JocheApp
Hellow
Nawasalimu watu Wa Mungu aliye Hai na wapambanaji katika changamoto za kila siku katika ulimwengu huu uendao kasi na mambo yake.
Hongereni wote waliotoka makazini lakini ambao bado wako makazini ama umeajiriwa au umejiajiri hiyo ni kazi yako.... lakini pia niwapongeze wanafunzi wote wale walio katika mfumo wa kikanuni yaani rasmi wa kukaa darasani na hata wale ambao hawakai darasani lakini wanajifunza...
Nisiwasahau kuwasalimia na kuwatia moyo wale ambao hajapata cha kufanya maana wanaona hana kazi wala hawasomi.... nina neno moja Kwenu FANYA KAZI YOYOTE malipo/faida ni kama ZAWADI usikubali kukaa bila kuwa na lakufanya.
Jioni ya Leo nina jambo moja natamani kukuambia nalo ni:-
USIPOTEZE TUMAINI KWA JAMBO/MAMBO ULIYOYAPATA LEO, HUWEZI IJUA SIKU YA KESHO INAVITU GANI
Hapa kwenye tumaini ni eneo la msingi sana kama kijana kuwa nalo.
❗️Haijalishi uliuza Ubuyu ukaharibia dukani haukuisha na leo umeenda umekuta umeshatia ukungu. usivunjike moyo inua moyo wako jipe TUMAINI kesho ipo usikate tamaa.
❗️Haijalishi ulifuga mifugo ikafa au walivunja wakaiba na kuondoka nayo, usikate Tamaa Jipe Tumaini Kesho inakuja inuka na anza hapo ulipokwamia utavuka tuu.
❗️Haijalishi ulilima na mvua zikagoma, piga hesabu zako upya anza tena usipoteze Tumaini kesho inakuja.
❗️Haijalishi shule inakwama na unapata matokeo ambayo sio mazuri suluhisho sio kuacha ila kaza mwendo ungeza bidii utavuka
HUWEZI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOKUKABILI KWA KUTUMIA AKILI/NJIA/MPANGO ULE ULE ULIOLETA HIYO CHANGAMOTO
Maana yake ni nini?
✍🏼Ili uweze kuvuka changamoto inayokufanya usisogee mbele ni lazima utafute maarifa ya zaidi kuliko changamoto inayokusumbua na kukufanya usipige hatua.
✍🏼Soma Vitabu vyenye mlengo wa eneo ambalo unafanya litakusaidia kukuimarisha na kukuinua zaidi
✍🏼Soma Biblia chakula cha Nafsi/Roho ili kuiimarisha roho yako isimame upya kwa ujasiri mpya na Roho wa Mungu akiwa Pamoja nawe.
✍🏼Epuka Marafiki wasio na faida katika maisha yako.
✍🏼Pata muda wa kujikagua kwa kila hatua unayopiga katika Maisha yako.
NIKITAKIE SIKU NJEMA NDUGU YANGU.
NEVER LOSE HOPE, TOMMOROW IS COMING TUKUTANE KESHO TENA MUNGU AKITUPA UZIMA.
JocheApp
————————————-
Author: Joseph G. Mrema
Contacts: 0712 851687
Email: josephgeotham4@gmail.com
www.jocheinc.blogspot.com
————————————-
JocheApp
No comments
Post a Comment