MATOKEO (RESULTS)!!

Imeandikwa na Joche wa JocheApp

Matokeo ni majibu/zao/tarajio/tunda ambapo hupatikana baada ya kupitisha kitu fulani katika mchakato ambapo mchakato huo unakuwa na lengo la kuzalisha hilo jambo ambalo umelipata.

Mfano: 
Binadamu ni tokeo linalotokea mara baada ya Binadamu Mume na Mke kukutana.

Tunda ni tokeo la mbegu kuoteshwa na kuota nakadhalika

Katika mchakato wa kutengeneza matokeo kuna mambo ambayo huweza jitokeza kama tokeo nayo ni Tokeo Hasi na Tokeo Chanya.

Watu wa Biashara huweza kusema kuwa tokeo hasi ni hasara na tokeo chanya ni faida.

Kwa wakulima ukisema tokeo hasi ni mazao ambayo hayajaweza kumea vyema shambani na kutoa matunda au nafaka ambazo hawakuwa wamezitegemea lakini pia tokeo chanya ni pale shamba linapomea na kuzaa matunda na nafaka zikawa zenye afya.

✍🏼Kwanini naongelea Matokeo/Results?

Kwa mtu awaye yeyote tokeo la kitu namna lilivyo ndio linathari kubwa sana katika utekelezaji/ufanisi wako kwa jambo husika.

Hii wengi tunaweza tusifahamu hapa.. Unakumbuka kipindi upo darasa la Pili au la Tatu ukataja orodha(table ) ya pili na ya tatu wakati darasa zima kukiwa hakuna mwingine aliyeweza.

Kwa ambao waliweza watakuwa mashahidi iliwapa nguvu ya kupenda hesabu lakini walioshindwa wengi walianza kuichukia hesabu kwa kuona ni mzigo na ngumu..

Unakumbuka ulipofaulu mtihani wa midterm ukikupa speed ya kufanya vizuri katika mitihani iliyofanya kwa kiongeza speed zaidi na kuongeza nguvu zaidi.

✍🏼Nini sasa nataka kusema?

MATOKEO ya kitu unachokifanya ni muhimu sana kwa mafanikio yako....

Unapopata matokeo chanya basi ni dhahiri inakuongezea nguvu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi na kusonga mbele zaidi. 

Unapopata matokeo chanya shauku ya kufanya zaidi na kufanikiwa zaidi inakuwa kubwa 

Unapopata matokeo chanya uwezo binafsi wa ndani hukua na kuchangua kiasi cha kuibua na vipaji vingie ambavyo vipo ndani yako na hukuwahi dhani kuwa unaweza kufanya.

Unapopata matokeo chanya kujiamini kunaongezeka ndani yako kwa kiwango kikubwa sana na kupelekea kufanya vizuri zaidi.

Na matokeo ya Matokeo hasi basi ni kinyume cha hayo ya matokeo chanya.

✍🏼CHA KUSHANGAZA

“Hakuna binadamu ambaye anataka matokeo hasi lakini wengi wetu tunafanya mambo ambayo yanakaribisha matokeo hasi”

Vipo vitu vya msingi vya kuzingatia ili uweze kupata matokeo chanya katika jambo lolote unalolitaka.



Vitu hivyo ni kama ifuatavyo:

1. FANYA KILA JAMBO KWA KUSUDI

Kabla hujachukua hatua ya kufanya jambo lolote kwanza hakikisha unajua matokeo tarajiwa ya jambo hilo. Mfano: unapotaka kukata mti kwenye shina wakati unataka kupata tunda katika mti huo siku za usoni utakuwa hujajua nini unachokifanya muda huo lakini ukichukua hatua ya kuumwagilia na kuuwekea mbolea maana yake unatengeneza mazingira ya kupata tunda katika mti huo siku za usoni.

2. TAFUTA MAARIFA SAHIHI YA JAMBO UNALOTAKA KULIFANIKISHA

Maarifa ni mengi sana ambayo mtu unaweza kupata katika mambo tunayoyafanya lakini cha muhimu zingatia maarifa sahihi.

Tujua samaki hukaa ndani ya maji ni kweli. Lakini ni muhimu kujua samaki huyu ninayemfuga je anaishi katika maji ya aina gani? Ya baridi au ya chumvi? Ninatakuwa kuwa Docta (ndio ndoto yangu) basi soma vitabu vya kukupeleka kuwa docta. Na kwa namna hiyo basi utaweza kufikia tokeo Chanya kwa urahisi zaidi.

3. FANYA JAMBO HILO MARA KWA MARA KWA VITENDO

Kiuhalisia kufanya mambo kwa vitendo hukaribisha matokeo chanya kwenye maisha yako. Hasa jambo lile unalolitaka. Kama ni mwanamichezo utaambiwa fanya mazoezi mara kwa mara, kama ni mfanyabiashara utaambiwa tu fanya biashara bila kuchoka. Usichoke usikate tamaa. Kama ni darasani utaambiwa fanya mazoezi mengi katika somo hilo, kama ni uandishi utaambiwa fanya kwa vitendo kama ni uimbaji fanya zoezi. Kufanya zoezi kwa vitendo ni dhahiri tokeo chanya litajidhihirisha.

4. USIENDEKEZE UDHAIFU WAKO AU MASHAKA

Ni kweli kwenye maisha tunatofautiana mitazamo, tunatofautiana fikra, tunatofautina viwango katika nyanja zote. Wapo wanaoweza zaidi na ambao bado wako katika kiwango cha chini.

Pamoja na hayo usiendekeze udhaifu huo kuwa ndio sababu ya wewe kushindwa kufanya jambo katika maisha. Wapo watu wamefanya makubwa pamoja na udhaifu wao. Kwanini mimi na wewe tushindwe kuyavuta mambo chanya kwenye maisha yetu? Je ni hofu na woga ndio vinatutisha? Ni lazima kusonga mbele na kuvuta vitu chanya yaani matokeo ili kuweza kusonga mbele.

5. JIPENDE NA JIKUBALI
Kujipenda ni zaidi ya kuvaa mavazi ya gharama, vito vya thamani au hata kula vitu vya bei fulani katika maeneo fulani ya gharama. Unapozungumzia kujipenda katika dhana ya mtu mwenye maono ni kutambua nini anataka na anajipa kipaumbele kiweze kutimia katika maisha yake. Na sio kutimiliza tu bali kutimia katika kiwango kilichotukuka. 

Katika upande wa kujikubali ni kufahamu kipi unaweza kukifanya kwa kiwango na kipi huwezi ili kupata msaada kufanikisha kwa namna ambayo itavuta tokeo chanya katika maisha yako.

Usingoje mtu akukubali au kupende. Anza wewe na wengine watakukuta njiani umesonga.

🔮Kwa Makala zaidi za kukuelimisha USISAHAU KUDOWLOAD Application inayoitwa JocheApp (inapatikana katika Playstore) katika simu yako.

JocheApp
————————————-
Author: Joseph G Mrema
Contacts: 0712851687
Email: josephgeotham4@gmail.com
www.jocheinc.blogspot.com
————————————-


17/08/2018

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...