UNATAMBULIKAJE?
JE UNATAMBULIKAJE?
Imeandikwa na Joche na imeletwa kwako na JocheApp
Habari Ndugu msomaji wa Makala zetu
Mwanafalsafa mmoja ajulikanae kwa jina ka Stuart Wilde aliwahi kusema kwamba, “Ufunguo wa Mafanikio katika maisha ya Mwanadamu ni kuunganisha nguvu zake katika kutekeleza yale aliyojipangia kufanya, pindi utakapofanya hivyo, watu watavutiwa na na wewe, na watakapoonyesha kukuelewa na kuvutiwa na wewe basi walipishe”.
Ni kafalsafa kadogo sana kwa mtazamo wa haraka lakini kwa namna ya kiuchambuzi ni jambo pana sana.
Unaweza kuwa na malengo mazuri lakini kama usipoweka nguvu zangu katika hayo malengo yako ni vingumu watu kukuona na kuona matunda ya kile unachokifanya na kuvutwa kuja kutaka huduma au kutaka bidha ambayo unaiuza.
Naongelea sana kwenye upande wa biashara lakini kuna maeneo mengi sana.
Mfano: Ulikuwa mwanafunzi mahali ukaunganisha nguvu na maarifa watu wataona tu hata ukimaliza watakuchukua tu kwa uharaka ule ule...
✍🏼Nguvu ni nini?
Ni namna unavyojibidiisha katika lile jambo lako au lile umepewa kulitekeleza kwa wakati huo.
✍🏼Jambo lingine ambalo ni muhimu kulifahamu ni namna gani unapanga mambo yako?
Mpangilio wa mambo ni jambo la muhimu sana kwa mtu ambaye anataka kufika mbali kiuchumi au hata kitaaluma au kiuongozi.
Utajuaje uko katika mpangilio wa mambo yako?
Jikague tu katika masaa 12 yaliyopita leo umefanya nini? Na katika hayo uliyotenda yanachangia kwa kiasi gani wewe kufikia malengo yako? Je yanafika haya asilimia 50 ya uliyoyafanya leo?
✍🏼Vipi watu uliojumuika nao wanachangia kwa kiasi gani katika safari yako ya malengo uliyojiwekea?
✍🏼Vipi kuhusu sehemu ulizoenda zinachangia kwa kiasi gani katika jambo lako unalotaka kulifanya?
N.k
🌐Tunaishi katika Dunia yenye mambo mawili mawili (duality).
Mfano: kuna juu na chini, mwanga na giza, joto na baridi, ndani na nje, haraka na polepole, kushoto na kulia.. hii ni mifano michache sana ipo mifano mengi sana sana.
Ili jambo moja liwepo ni lazima la pili liwepo pia yaan yanategemeana.
Huwezi sema hii ni nyepesi kama hakuna nzito.
Hivyo basi ni muhimu sana kutambua kama huweki bidii katika lile unalolitaka basi tambua unajijengea mazingira ya kufeli na kushindwa.
Unajijengea mazingira ya kukwama hapo mbeleni au hata kutumia njia ambazo si halali ili uweze kufanikisha jambo unalolitaka.
Mwisho:
Chagua jambo moja unalolitaka au mawili au matatu kutegemea na uwezo ulionao.
Usiende tu kila kitu unataka kufanya ama la utaishia njiani.
Yaani ukisikia NETWORK MARKETING zinalipa na wewe huyo mbio unawekeza, ukisikia Utengenezaji wa Sabuni unalipa na wewe hiyo upo hujafanya kwa muda hata kidogo umehamia karanga, mara unga mara kilimo mara duka..
Yaani hueleweki kila kitu unataka wewe.
Usipoeleweka hivyo hata jamii itashindwa kukuelewa na mwisho hawatakuwa wanavutiwa na mambo yako coz hawajui wakufate kwa lipi kila kitu unafanya na hufanyi kwa muda wala hufanyi kwa ukamilifu wala hufanyi kwa bidii.. unapapasa tu..
Sio sawa kufanya hivyo unapoteza UTAMBULISHO wako wa kiujasiriamali.
Fanya jambo ambalo litakutambulisha wewe kama wewe. Kama vile ukisikai Diamond unajua ni mwanamuziki, ukisikia Azam unapata picha ya Unga, Maandazi, Tv na kadhaliaka..
Fanya kitu kitakacho kutambulisha wewe kama wewe.. WEKA BIDII KATIKA HICHO UNAFANYA NA MATUNDA YAKE UTAYAONA TU.
Asante na uwe na wakati mwema
DOWLOAD NOW JOCHEAPP
——————————————-
Mwandishi: Joseph G. Mrema
Contacts: +255712851687
Email: josephgeotham4@gmail.com
Blog: www.jocheinc.blogspot.com
——————————————-
No comments
Post a Comment