AMUA KUFANYA UNACHOTAKA KUFANYA

AMUA KUFANYA UNACHOTAKA KUFANYA

Hongereni na poleni na mihangaiko ya siku nzima ya leo...

Zaidi ya yote nikukaribishe katika makala za kila siku ambazo mlengo wake mkubwa ni kubadilisha mitazamo yetu lakini pia kuongeza hamasa ndani yetu katika harakati za kimafanikio katika mambo yale ambayo tunayafanya na kuyajenga kila siku ili kufikia kilele cha mafanikio.

(Ushuhuda wangu Binafsi)

Siku ya Leo naomba kuchukua nafasi ya kuwashukuru ninyi nyote na Mungu pia kwa kunisaidia kufanikisha ambayo nilikuwa nimejiweka..

Lengo langu ilikuwa ni kuanzisha BLOG katika mwezi huu na katika kuanzisha huko nilijiwekea lengo la kufikisha japo WAPITIAJI/WASOMAJI/VIEWERS 1000 katika mwezi wa kwanza tola nilipoianzisha..

Na Mungu amejibu kwa kuwagusa watu mbali mbali kwa kupitia na kujifunza katika BLOG hiyo....

Leo ni WIKI MBILI na siku TATU tayari BLOG yangu imeweza kufikisha VIEWERS 1000 na zaidi... hii ni pongezi kwako lakini pia pongezi kwetu sote kwa namna mlivyoonyesha kunisapoti....

Wapo watu waliosaidika kupitia Blog hiyo... lakini pia wapo waliosaidikika kupitia Facebook Account yangu na wengine katika Magrup ya Whatsapp...

Pongezi hizi ni kwenu nyoote..

Maana napokea meseji za kawaida, whatsapp, facebook meseji na Comments, Emails, Calls kwa kutoa ushuhuda jinsi zilivyowagusa na utukufu wote Namrejeshea Mungu.

Wakati naanza haikuwa kazi rahisi wapo walionicheka, na wengine waliniambia Joche hakuna atakayekuja katika blog yako zipo Blog za hadithi zipo za michezo na za udaku na miziki..

Lakini nilijipa moyo... nikajifunza kutengeneza Blog yangu na wapo ndugu walionisapoti ili kuisimamisha isogee na iwe na muonekano mzuri....

Na hivi ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku..... wapo watakao kukatisha tamaa kuwa haiwezekani, wapo watakao kuangalia tu kama hawaoni unavyohangaika lakini kamwe huwezi kosa atakayesapoti lile unalolifanya...

Anza kufanya hata kwa kidogo na hata kwa unyonge kuna mtu yuko pembeni anasubiria kukusapoti lakini mpaka uchukue hatua kwanza....

Pasipo hatua pasipo kuanza huwezi sogea utabaki ulipo...

Kama ni mwanafunzi hatua inahitajika ili kufikia malengo

Uwe ni mfanyakazi hatua inahitajika ili upande kiwango cha mshahara na cheo pia

Uwe ni mfanyabiashara pia hatua inatakiwa kuanza ndipo ufikia pale unapotaka...

Usiogope maneno ya watu, usiogope kimya cha watu, usiogope nyimbo za watu....

Anza sasa, fanya inawezeka hata kwako ni wewe tu kuamua kuanza... hilo unalowaza kila siku lifanyie kazi

Usitishwe na wavivu, Usitishwe na waliokata tamaa...

Maana stori ni nyingi fulani alifanya akashindwa, na yule alifanya akakwama....

Sasa ni wakati wa wewe kuandika historia yako kuwa wao walishindwa ila wewe uliweza...

Usikubali akili za walioshindwa kufisha malengo yako....

Lazima ung'ang'ane, lazima uchimbe, lazima ushikamane mpaka ufikie malengo yako...

Mpaka tokeo ulilotaka lionekane limeonekana...

Jana ulishindwa na ukapata somo, na kesho inakuja utujie somo hilo la jana kutokurejea makosa....

Kushindwa sio kosa ni somo... kosa ni kuacha kufanya baada ya kushindwa...

Mwisho:

Mtazamo chanya hujengwa na mtu binafsi pale anapoamua... kama usipoamua hata iweje ni vigumu kubadilika mtazamo wako wa ndani.... Kukubali kushindwa ni rahisi kuliko kujikusanya kwaajili ya kupambana baada ya kushindwa.... JIPE MOYO... mafanikio yako yanategemea sana na wewe mwenyewe sio Rafiki wala sio Mzazi ni wewe mwenyewe.... Amua sasa... Pambana sasa... Jitenge na Uvivu... Jitenge na mambo yasiyokupeleka katika Malengo yako.....

Na hatima yake UFIKIE KILELE CHA MAFANIKIO YAKO....

AMEN
_________________________________________________

JOSEPH GEOTHAM MREMA
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc

Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp&Calls: +255 (0) 712 851 687

Visit my Blog: www.jocheinc.blogspot.com

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...