SI KILA FURSA NI YAKO
Poleni wote wanaopenda mabadiliko chanya katika maisha yao ya sasa na ya baadae lakini pia wapenda mabadiliko katika maisha yao kwa mihangaiko ya siku nzima....
Humu duniani kila siku watu hugundua fursa mpya nyingi kila siku iendayo kwa Mungu
Na fursa hizi wapo wanaozifanyia kazi na wengine hutumia kama mtaji wa kuwanufaisha wao ili kuleta mabadiliko ndani ya maisha yao.
Mfano: Wakati wengine kufundisha ni kipaji lakini wengine hujinifaisha kwa vipaji hivyo kwa kuwaendeleza wenye vipaji ili waweze kunufaika (watu hawa huitwa mameneja)
Ukimtazama Meneja yeye hafundishi, haimbi, hachezi lakini kaona fursa hapo kati anajinufaisha..
Lakini wapo waliokuwa na vipaji hivyo na wakajiendeleza na wakafika mbali sana kimafanikio...
Sasa
Katika maisha hayo ya kuchangamkia fursa na kuzifanyia kazi kuna kitu cha msingi lazima ukifahamu
1. Si kila fursa inayopita mbele yako ni ya kuirukia (tambua kwanza nini unataka kwaajili ya nini na kwa muda gani na kwanini unaitaka fursa hiyo)
2. Katika kuchangamkia fursa kuna gharama ya kujifunza na kuiboresha ili kuona kuweza kuwa na utofauti kati yako na mwingine...
(Sote twaweza uza matunda lakini utofauti huja ni namna gani matunda hayo tunayauza??? Kwa kiwango gani? Kwa utaratibu upi???
3. Katika kila Fursa kuna kushindwa na kuna kufanikiwa lakini kuna kuduma
(Haya hutokea si kwa bahati mbaya ila ni ili uweze kuongeza kiwango na ubora wa huduma au bidhaa unayotengeneza
Niweke mkazo
Kushindwa kwa lugha rahisi ni kuanza upya kwa fursa lakini kwa kiwango zaidi tofauti na awali...(Henry Ford)
Kwa kuona hili naomba nikutie moyo usiogope kushindwa, usiogope kuanguka.
Kwanini nasema hivi:
Ushawahi ona mtoto mdogo akitaka kujifunza kutembea?? Huanguka mara kadhaa na huumia lakini kesho utamkuta tena anataka kutembea japo bado ana makovu na vidonda vya jana haviwazii hivyo mwisho wa siku anatembea...
HII TABIA KILA MMOJA WETU AMEZALIWA NAYO
Swali la Msingi:
Hii roho/moyo wa kutokukata tamaa ambayo tumezaliwa nayo imeenda wapi???
Hebu turejeshe ule moyo wa utotoni wa kutokukata tamaa
ZINGATIA HILI
Kama unataka kuwa na matokeo chanya katika maisha yako epuka sana kukaa na watu wenye mitazamo hasi (hata kama ni rafiki kipenzi) maana watu wenye mitazamo hasi ni vigumu kupata matokeo chanya...
Mwisho:
Ninachofanya hapa ni kukoonyesha wapi pa kuangalia ila kitu cha kuangalia ni wewe mwenyewe kuamua...
"The Best Teachers are those who shows where to look but dont tell you what to see" -Alexandra K. Trenfor
_______________________________
JOSEPH GEOTHAM
Founder of JOSEL COMPANY
Joche Inspirational and Motivational Inc
josephgeotham4@gmail.com
+255 (0) 712 851 687
Follow me kwa
👉🏼Tweeter
👉🏼My Facebook Page: Joche Inspirational and Motivational Inc
SHARE na kwa RAFIKI YAKO
No comments
Post a Comment