UKICHAGUA JAMBO KUBALI NA WAJIBU ULIOAMBATANA NA JAMBO HILO

Napenda kuchukua muda huu na wasaa huu kukusalimia na kukukaribisha katika moja ya makala zetu zinaendelea kuja kwako ndugu rafiki na mwanaharakati wa mipango malengo yetu kimaendeleo na hasa zikiwa na mlengo wa kuongeza hamasa kuelekea kilele cha mafanikio yetu ya maisha yetu
Hali tukiwa ni wanamapinduzi katika maisha yetu kila mtu anaeneo analoona kuwa kwa upande wake litamletea mabadiliko halisi katika maisha yake au katika lile jambo ambalo analolifanya ndani ya maisha yake, ambapo wengi huwa tunaita ni malengo au ndoto.
Na katika kuelekea katika ndoto hizi huwa tunafanya kuchagua kipi cha kufanya na kipi ambacho si cha kufanya ili niweze kufika kilele cha mafanikio yangu...
MFANO: Kama unataka kuwa mwimbaji mzuri lazima uwajibike katika kujifunza muziki lazima uwajibike kufanya mazoezi ya kuimba na viungo ili kuwa katika ubora wa sauti njema na yenye afya lakini pia yenye nguvu na yenye kuvutia unapaswa kuacha vitu vyoote vinavyochangia katika kuharibu sauti yako....
Huo ni mfano wa mtu anayetaka kuwa mwimbaji mahiri wa nyanja yoyote...
Hii inamaana gani... katika kila jambo unalotaka kufanya kuna kuchagua na katika kuchagua kuna gharama lazima uzipitie ama kwa kutaka au kuto kutaka gharama hizo ziko pale pale....
Watu wengi tunapenda kufikia kilele cha mafanikio lakini hatuna muda na kutekeleza wajibu wa vile tulivyovichagua...
Tambua pale ulipokubali kuwa mwanasheria/Mchumi/Mjasiriamali(Mfanyabiashara)/Mwanamichezo/Mwajiriwa/Baba/Mama/Kaka/ na kadhalika kuna wajibu nyuma yake...
Hivyo mafanikio yako yanafungamana na namna ile ambayo utaitumia katika kutekeleza wajibu wa kile umechagua....
Hujawahi kusikia Kaka fulani jamani ni Jembe katika eneo fulani... tambua huyo mtu ametambua kitu alichochagua na ametambua wajibu wake katika kile alichochagua...
Vijana wengi hatuna muda wa kutekeleza wajibu wa kile tumechagua au tumepewa...
Utakuta mtu ni mfanyakazi lakini kazini anachelewa, muda mwingine anatoroka, Hakamilishi ripoti kwa wakati, anakula rushwa, hatoi huduma stahiki kwa wakati stahili... kama uko hivyo inakupasa ubadilike ili kuleta mabadiliko katika maisha yako na kutendea haki wajibu wa kile umechagua
Kama ni Mjasiriamali vivyo hivyo.. acha kuamka saa tano kwa vile huna kitabu cha kusaini... tambua wajibu wa ulichokichagua... maana pia mafanikio yako yamefungwa hapo katika wajibu wa ulichokichagua.... kushindwa kutambua wajibu kunakufanya kutumia nguvu nyingi na njia nyingi ambazo mara nyingi huwa si halali kufikia malengo yako...
Unapofanya maamuzi ya kuwa na familia ili hiyo familia iwe katika muundo bora na maisha yenye amani ni lazima ukubali wajibu utakaoubeba kama baba/mama wa familia usipoubeba wajibu huo basi huwezifanikiwa kwa kiwango kilichotukuka hasa katika malezi ya familia na hata katika kuigharamia na kuihudumia familia.
Vivyo hivyo katika mahusiano(uchumba/urafiki), ili kuyafanya yadumu na kufikia mafanikio na malengo mliyojiweka ni muhimu kila mtu kutekeleza na kutambua wajibu wake ili kuleta mafanikio na ubora wa mahusiano hayo.
Ndivyo ilivyo na katika nyanja zingine. Pindi utakapotambua wajibu wako na kuutekeleza basi mafanikio ni dhahiri... ila usipotekeleza wajibu katika nyanja uliyochagua basi kushindwa kwako ni dhahiri....
Mwisho:
Amka sasa... Jikague leo.. Fungua macho yako na masikio yako na akili na ufahamu pia ili uweze kujua wajibu wa vile umechagua kuwa katika maisha yako...
Hakuna jambo jepesi lakini hakuna jambo gumu kama umeweka SHAUKU yako katika eneo hilo utapata majibu ya maswali yako kwa wakati na mwisho utapata mpenyo wa kufikia kilele cha maisha yako...
Kijana jitambue na ifanye jamii yako kukutambua wewe umechagua kuwa nani na itakusapoti lakini mpaka wewe ujitambue na utambue wajibu wa kile wewe umekichagua...
AMEN
_________________________________________________
JOSEPH GEOTHAM MREMA
Founder of JOSEL COMPANY
Joche Inspirational and Motivational Inc
Contact Us:
Facebook: Joseph Geotham Mrema
Fb Page: Joche Inspirational and Motivational Inc
Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp&Calls: +255 (0) 712 851 687
Tembelea Blog yetu:
www.jocheinc.blogspot.com

No comments
Post a Comment