PIGA HATUA MOJA NYINGINE ITAFUATA TU

PIGA HATUA MOJA NYINGINE ITAFUATA

Habari yako ndugu??

Nikukaribishe katika makala hii itakayokuongezea mtazamo chanya ndani ya maisha yako.

Nianze kwa kuwapongeza Watanzania wote, "Hongereni kwa kusherehekea sikukuu ya Nanenane... yaani sikukuu ya Wakulima"

Lakini pia niwapongeze wakulima wote ambao wapo humu na wanaotamani kuwa wakulima siku moja katika maisha yao..

Leo nataka kukuhamasisha jambo moja ndani ya moyo wako na ndani ya maisha yako ambalo ni muhimu...

Katika maisha yetu ya kila siku tunakuwa na mambo tunayaona tunatamani kuyafikia na tunatakamani kuyamiliki au kuona yanakuwa sehemu ya maisha yetu...

Pamoja na kutamani au kutaka huwa tuna vitu hatutaki kuviona vinatokea katika maisha yetu... ambavyo muda mwingine hutukwamisha kusonga mbele

Ngoja nikuambie kitu kimoja...

Kuna aina ya watu wanaogopa kufanya jambo aidha watachekwa na watu kutokana na elimu zao, nyadhifa zao, umri wao, au hata uzuri wao...

Lakini kwa kuogopa huko wamebaki katika eneo hilo la kutaabika kwa kufa na tai shingoni... wakati wana jambo la kufanya ambao lingeweza kuwatoa hapo walipo na kusonga mbele...

start moving forward

Pia katika maisha kuna aina ya watu wao ni wanapanga tu mipango ila utekelezaji wa mipango hiyo hawajahi kuanza hata siku moja kwa kuogopa au kughairisha mambo..

Jambo ambalo ni sumu kubwa kwa mwanamabadiliko na mwana harakati

Wengine tunaogopa kufanya au kuzifanyia kazi ndoto zetu kwa kuogopa changamoto ambazo tunaziona kwa wengine au tumezisikia kwa watu wengine ambao wamekuwa wakifanya vitu kama vile sisi tunatamani kufanya katika maisha yao na hili limekufanya kughairisha maamuzi yako na mipango yako kila siku kwa kutazama waliokwama zaidi kuliko waliofaulu kupitia jambo hilo


TAMBUA

Hakuna meli iliyotengenezwa ili ikae bandarini tu...

Hivyo wakati Mungu anakuumba wewe kuwa wewe ulivyo alitaka uje ulete mabadiliko katika dunia hii..  hivyo kutokufanya jambo sio sahihi au kuogopa kufanya jambo si sahihi... anza hapo ulipoooo....

Mtaji

Wengi hulia juu ya mtaji sina...
Ukiangalia watu wa namna hii ukimuuliza je ukipewa milioni 10 muda huu utafanyia nini?? Hata majibu yake ni ya kusuasua...

Maana yake kikwazo sio MTAJI...

Kikwazo ni uchache wa maarifa...

Jifunze kuanza kidogo lakini ukiwa na ndoto kubwa...

Na hili ni jambo la msingi sana..

Kwa kuanza kidogo utaweza kujua mzunguko wa kile unachokifanya lakini pia utafahamu changamoto zake taratibu na marekebisho yake utafanya kwa urahisi wakati unaendelea kukua taratibu hata kama unamtaji mkubwa anaza kidogo kidogo huku ukuendelea kukua taratibu...

Utakuta mtu hajawahi kulima hata siku moja lakini ana taka aanze kilimo cha hekari 50 huko... Nafasi za mtu huyu kufail ni kubwa sana kuliko kufanikiwa

Hivyo anza taratibu huku ukikua na kukomaa mpaka utafikia ndoto zako pale unataka kufika....

Wakati huu natamani kukuuliza swali la msingi;

1. Unataka kuwa mtu wa aina gani?

2. Ndoto yako ni ipi na umeshaifanyia kazi kiasi gani mpaka sasa?

Kitu mtu anataka kufanya ni kile kimemjaa ndani yake mwenyewe na shauku yake kule ilipo....

Mfano:

Ukiona mtu anashona nguo ww unajisikiaje??
Ukiona mtu anafundisha je??
Ukiona mtu analima ww unajisikiaje??


Hizo ni baadhi ya vitu, kama unaona shauku yako kubwa iko upande wa kilimo basi fanyia kazi eneo hilo...

Tafuta walio katika eneo hilo la kilimo (waliofanikiwa ili kupata taarifa sahihi na watakuonyesha njia za kufanikiwa kuliko kuuliza walioshindwa)

Tafuta maarifa katika vitabu..

Panga mpango mkakati juu ya kufanikisha hilo..

Jifunze kufanya kwa Vitendo vile vitu unatamani vitokee katika maisha yako...

Kuwa na shauku isiyokatika wala isiyoyumba yumba....

Tengeneza vyanzo vingi vya fedha kwa kadri uwezavyo ili uweze kufanikiwa kwa haraka.... hata kama ni vidogo ila kwakuwa vipo vingi vitakuletea mawazo chanya....

ANZA SASA

Usiogope kuanza usikatishwe tamaa katika kuanza safari yako hakikisha kila siku unasogeaa usiogope speed ya kuanza au kutembelea..

Kama hutaweza kwenda kwa speed ya kuruka basi kimbia, kama hutaweza kukimbia basi tembea na kama hutaweza kutembea basi tambaa yaani ilimradi unasogea katika safari yako na hutabaki kama ulivyo.....

REMEMBER...

"A winner is a dreamer who never give up"

DONT GIVE UP

DONT LET IT GO

DONT GET TIRED...

PUSH TILL ITS HAPPENING.....

Hakuna safari isiyo na vikwazo....

Usipoanza jambo siku zote utaona ni gumu.. lakini ukianza utaona ni jepesi sana sana na linawezekena kwenda mbali zaidi....

Mfano: Ukimuona mtu anapiga Kinanda unaweza ona anafanya miujiza... lakini ukimuuliza yeye atakwambia si hivi na hivi tu bonyeza tu hapa na hapa.. lakini kwa vile hujui utaona ni mzigo bado...

Hivyo anza kufanya sasa.

Na Mungu akubariki sana sana kwa kusoma makala hii..

TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE..


____________________________________

Joseph Geotham
Joche Inspirational and Motivational Inc
Founder of Josel Company
josephgeotham4@gmail.com
+255 (0) 712 851 687

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...