TABIA AMBAZO UNAPASWA KUZIACHA ILI UWEZE KUFANIKIWA

TABIA AMBAZO UNAPASWA KUZIACHA ILI UWEZE KUFANIKIWA

Habarini za kazi na shughuli za siku nzima ya leo...

Nipende kukukaribisha katika moja ya mfululizo wa makala zetu. Sasa karibu tuendelee na makala hii:-

Kwanza kabisa nianze kwa kusema katika maisha tunayoishi ya kila siku kila mtu anatabia zake na mwenendo wake ambao huo ndivyo alivyo yaani na wengi wetu tunakuwa na tabia hizo ama kwa kujifunza au kufundishwa hasa kutokana na malezi na jamii inayotuzunguka katika maisha yetu

Haijalishi tabia hizi ni nzuri au mbaya...

Maaana leo siendi upande huo wa huko.. nataka kuzungumzia upande mwingine kabisa....

Leo nataka kuzungumzia tabia ambazo ili uweze kusonga mbele kufanikiwa katika jambo lolote... iwe KIROHO AU KIUCHUMI AU KIMWILI au namna yoyote ile ni lazima UZIACHE

Maana mafanikio yako au kufeli kwako na kiwango chake inategemeana sana na Tabia ambazo unazotembea nazo kila siku

Moja kati ya Tabia hizo ni

KUTOA VIPAUMBELE ZAIDI KWENYE STORI NA HADITHI KULIKO KWENYE UKWELI HALISI

Hili jambo linatukumba watu wengi sana..

Huwa hatupendi sana kufuatilia ukweli wa jambo ambalo tunataka kufanya au kuliona linafanikiwa na kujikita zaidi kwenye stori au hadithi ambazo hazina ukweli ndani yake...

Kuna muda huwa tunaambiwa mambo ya msingi ya kutuvusha ila hatupendi tunapenda sana kupewa hadithi zinazotupa moyo na zinazotupamba...

Jambo la Muhimu epuka tabia hii..

Fuatilia ukweli wa jambo fanya kulingana na taratibu zake na utaona mafanikio yake...


Tabia ya Pili

KUTOKUTOA NAFASI YA KUKOSOLEWA

Eneo la kukosolewa watu wengi sana hatupendi... hata kama mtu anajambo lake anafanya akikosolewa basi atasusa au ataacha kabisa au atakuwa mkali kupitiliza...

Muda mwingine ili uweze kupanda au kufanikiwa kutoka eneo ulilopo kubali kukosolewa pasipo kujali uchungu wa kukosolewa huko au mapana ya kukosolewa huko..

Watu waliofanikiwa walikosolewa na kusahihishwa mara nyingi sana.. na ndio maana tunawaona wako hivyo walivyo na wanaboresha huduma au bidhaa zile wanauza au kutengeneza...

Jambo la Muhimu epuka tabia hii...

Unapokosolewa tambua watu hao wanataka ufanikiwe zaidi na ufike mbali zaidi katika kile unafanya...

Tabia ya Tatu

KUJIAMINISHA KUWA UKOSAHIHI ZAIDI KATIKA UNACHOKIAMINI KULIKO WENGINE

Ni kweli katika maisha ni muhimu sana kuamini kile unachokifanya na kukiwekea mkazo hata kama wengine hawaamini kuwa kinawezekana...

Mfano

Steve Jobs aliamini kuwa kuna uwezekano wa kuwa na camera na music players katika simu.. na alikifanyia kazi ikawezekana na alafanikiwa...

Lakini kuna wakati ni muhimu sana sana kusikiliza waliokutangulia wanaofahamu zaidi watakuonyesha njia katika kile unachoamini...

Hivyo imani yako juu ya mafanikio yako usizuie kusikiliza na wengine wanaamini nini vichuje vipime kama vinakusaidia chukua songa mbele na imarisha kile unachokiamini ili kiwe thabiti kabisa....

MWISHO: Tabia hizi tatu ni mfano ya Tabia nyingi sana ambazo hutukwamisha kufikia mafanikio yetu na malengo yetu yale tumejiwekea katika maisha yetu ya kila siku ambayo tunatamani tuyafikie...

Nikushukuru kwa kuungana nami muda huu katika makala hii..

Karibu tena


____________________________________

JOSEPH GEOTHAM MREMA
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc
Blog: jocheinc@blogspot.com
Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp & Calls: +255 (0) 712 851 687

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...