MAONO NA MAISHA YA URAFIKI
Hakuna asiyejua kuwa marafiki ni wa muhimu katika maisha na husaidia sana katika michakato ya maisha ya kila siku
Lakini marafiki pia ni watu hatari sana katika maisha pale ambao wanakuwa wako na ajenda zao katika mashimo ya mioyo yao
Usijibidiishe kuwafukuza na kuwadelete namba zao au kuwakimbia ila lipo jambo moja la Msingi nalo ni ISHI KATIKA KUSUDI/MAONO
UKIISHI KATIKA KUSUDI/MAONO
1. Hutachagua Rafiki ila KUSUDI/MAONO yatachagua Rafiki
2. Maono/Kusudi litakufanya kujua kipi cha kusema na kipi cha kutokusema
3. Maono/Kusudi litakupa mtu au watu wa kukuvusha ngazi moja kwenda nyingine
4. Maono/Kusudi litakupa mwanga mpya au maarifa mapya ya kulifanikisha
RAFIKI NI MZURI ila KUSUDI/MAONO ndio DIRA YA UZURI WAKO KATIKA MAISHA YAKO
2017-Maarifa Akilini, Speed Unyayoni
Br. Joseph Geotham Mrema
Joche Inspirational and Motivational Inc
No comments
Post a Comment