ISHINDE HOFU YAKO ILI UWEZE KUFIKIA MALENGO YAKO

ISHINDE HOFU YAKO ILI
UWEZE KUFIKIA MALENGO YAKO


Habari za wakati huu?

Napenda kuwasalimu sana ndugu zangu ambao Mungu amenipa kibali cha kushirikiana nanyi tena muda huu mambo machache sana..

Ni muendelezo wa makala za kugusa maisha yetu ya kila siku ambayo tunayaishi ili kuleta badiliko la ndani na nje pia..

Katika makala hii ya leo napenda kutembea sana au kukazia sana juu ya kuto kuruhusu hofu kuzishinda ndoto/maono yako katika maisha yako.

Hapo Mungu alipotuumba vitabu vitakatifu vinasema kuwa alitupa nguvu ya kushinda kila jambo lakini pia kufanikiwa kulikuwa ndani mwetu...

Mbali na hivyo kila mtu anandoto ya kuwa mtu fulani au kumiliki kitu fulani au kufanya jambo fulani....

Ni muda umepanga lakini wengi wetu hatujavianza kuviishi hivyo tunavyovitaka, au kama tunaviishi ni hatufanyi kwa speed ile ambayo hata sisi tusingetamani mtu mwingine afanye....

Haya yote ni hofu ya kushindwa ndio inayotusumbua....

Hofu ya kutotaka kuaibika...

Hofu ya kutotaka kufanya makosa...

Wapo ambao wana vipawa/vipaji vya kufanya mambo makubwa sana lakini hofu iliyo ndani yetu inazika ndoto zetu....

Hii inatupelekea kukosa watu mahiri wa kufikia malengo makubwa lakini pia kutoa majibu ya maswali na matatizo yaliyomo katika jamii yetu....

Ukitaka kutengeneza hela/fedha/kipato kwanza tafuta swali/tatizo lililopo katika jamii...

Ukishalipata swali/tatizo nenda hatua inayofuata ya kutafuta majibu yake...

Ukishapata majibu yake utakuwa umetengeneza mfereji wa kipato ambacho kitakuja tu kwasababu unamajibu.....

Lakini katika kutafuta majibu ni lazima uweke hofu chini, maana si kila jibu litakuwa sahihi katika swali/tatizo lililopp katika jamii...

Hivyo jaribu jaribu  mpaka uone limetokea...  na limekuwa sahihi....

Ukiangalia watu waliofanikiwa ni watu waliojaribu kujibu maswali/ au kutafuta njia za kutatua matatizo yaliyomo katika jamii iliyowazunguka....

Hivyo ni wakati wako umefika na wewe kuangalia pale unapoishi kuna jambo gani linasumbua jamii unaloweza kulifanya????

Je ni maji???
Je ni Duka la vitu mbalimbali??
Je ni matunda???
Je ni bites??
Je ni genge???
Je ni Usafiri???
Na kadhalika...

Ukipata tu Swali hakikisha na Jibu unalipata haraka na ukilitendea kazi utaona mabadiliko...

Mwisho:

Usikubali Hofu izike ndoto zako...

Jitenge na Hofu...
Weka woga chini, inua tumaini jipya ndani yako.. ongeza mwendo kuelekea mafanikio ya ndoto zako na Mungu atakufanikisha.

PULL UP YOUR SOCKS...

_________________________________________________

JOSEPH GEOTHAM MREMA
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc

Visit Me:

Fb: Mrema Geotham Joseph
Fb Page: Joche Inspirational and Motivational Inc
Whatsapp & Calls: +255 (0) 712 851 687
Email: josephgeotham4@gmail.com

Blog: www.jocheinc.blogpot.com

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...