WEWE NI SHUJAA WA MAISHA YAKO

Katika maisha kuna kupanga na kupangua...

Na kupanga huku hutegemeana sana na maarifa mapya uliyoyapata ama kwa kusikia au kusoma au kuona kwa wengine....

Lakini pia hata kupangua huja kwa njia kama ya kupanga...

Na katika kupanga maranyingi huegemeza sana upande ule wa kuboresha kile ambacho ulichokwisha kukianza

Mara zote ni watu wachache sana ambao huandika malengo yao na kuyafiatilia kila mara na kila siku na kuyaboresha au kuyapunguza ili kuona njia bora ya kufanikisha

Mara nyingi huwa tunaandika pale mwaka ukianzia lakini baada ya hapo huwa tunayaacha na kuendelea na mambo yetu.

Ukija mwaka mpya basi tunaandika tena na muda mwingine tunayarudia yale yale...

Ukitaka kujua haya jikague mwenyewe...

Utaona ni wachache sana sana mipango yao ile ya kuanza mwaka wanatembea nayo mpaka mwisho....

Tunaposema MWANAUME ni KICHWA cha familia na MAMA ni MWILI wa familia...

Inaaana zaidi...

Kama unashindwa kufanya kitu ulichokipanga mwenyewe je utaweza kuongoza kitu alichopanga mwanafamilia wako na kumsaidia?

Ni vyema sana kuwa na daftari ambalo unaandika mambo yako ambayo kila siku labla ya kulala unalipita na ukiamka asubuhi unalipitia...

Utashangaa mabadiliko yatakayo kuwa yanatokea katika kaisha yako

Na asikuambie mtu raha iliyopo kuona jambo ambalo ulilipanga ukalitimiza halafu ukaliweka tiki kuwa nimelifanikisha kama nilivyosema....

Toka nimeanza kupractice hili jambo la kukagua mipango yangu na nilipofanikisha jambo moja nikaweka tiki..

Nikawa napatwa na kiu ya kuhalikisha jambo lingine limekamilika na kuliwekea tiki... na lingine na lingine

nini namaanisha.

 WEWE NI SHUJAA WA MAISHA YAKO

Maisha ni vita ni mapambano ni zaidi ya game, ulicheza kwa akili unakuwa shujaa ulicheza kwa mipango unakuwa shujaa ukihituma kwa bidii unakuwa shujaaa...


BE THE HERO OF YOUR LIFE

Usingojee mpaka rafiki, jirani, ndugu aje kunyoosha maisha yako...

Nyoosha mwenyewe maisha yako wao wakitaka kuweka baraka zao watakukuta njiani unakimbia hivyo watakuongezea speed.....

USIRUHUSU katika maisga yako mwenyewe KUWA KAMA KONDOO, MBUZI NG'OMBE na wengineo kama hao ambao wao daima hufuata kule wanapopelekwa, hawabishi akisukuwa anaendaaa....

TUJIFUNZE Mfano wa MNYAMA Simba siku zote yeye ni kiongozi wa kila kitu chake, anahasira ya jambo lake, anapokuwa na Njaa hutafuta kwa hasira mpaka apate...

SIMBA NI KIONGOZI

na wewe kuwa Kiongozi wa Maisha yako...

usiyumbiashwe na mawazo finyu ambayo hayana mbolea katika mfumo mzima wa maisha yako....

JIFUNZE KUKAA na WATU wenye MTAZAMO CHANYA maana watakuambukiza mfumo chanya ambao utakuletea MATOKEO CHANYA KATIKA MIPANGO YAKO....

 IKISHINDIKANA LEO KESHO ANGALIA WAPI ULIKOSEA sahihisha MPAKA MATOKEO YAPATIKANE ya kile unataka...

NDIO MAANA wanamichezo/waimbaji/ na wengineo wengi wanafanya mazoezi kila siku hata kama walifungwa wanafanya zoezi wakishinda wanafanya mazoezi hawaachiiii

Swali la KWAKO

Wewe umeghairi mara ngapi walipokucheka wenzio? Walipokudharau wenzio? Wakasema haiwezekani???

KUMBUKA
Leo watakucheka kwa unachofanya kesho watabishana keshokutwa watakupa hongera na watasimulia jinsi ulivyoanza na walivyokutana na wewe wakati unaanza..

STAY GOOD.....

_____________________________________________

Joseph Geotham Mrema
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc
Fb Page: Joche Inspirational and Motivational Inc
Blog: jocheinc@blogsport.com
Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp+Calls: +255(0)712851687

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...