HARAKATI HAZINA KIKOMO
HARAKATI HAZINA KIKOMO
Hellow Mwanaharakati????
Nakusalimu mwanaharakati mwenzangu wa maendeleo hasa ya maisha yetu haya ya mwilini na rohoni..
Katika maisha yetu ya kila siku tunaona fursa na muda mengine fursa hizo hupita ama hutupita kwa kujua ama kutokujua...
...ni wachache sana wanaoweza daka fursa sahihi kwa wakati sahihi... wengi wetu huwa tunashtuka wakati muda umeshatuacha na wakati mwingine imeshatupita..
Kitu ambacho wengi wetu kunatushinda ni kufanya Chaguo sahihi kipi tunataka kufanya na kwanini tunataka kukifanya kitu hicho kwa wakati huo!
...uchaguzi sahihi utakufanya kupenda kitu unachokifanya maana kwa kufanya uchaguzi sahihi basi ni rahisi kuona njia unayoiendea na hata kama ukikutana na vikwazo ni rahisi kuona mpenyo wa kutoka katika changamoto hiyo...
Kuna Falsafa moja inayosema
"amua unachokiamini, amini unachokiamua"
Ukiona unaamua jambo kulifanya lakini imani yako haiko hapo jambo hilo likwepe liache usifanye maamuzi kabisa maana kwa kukosa imani ni vigumu kuwa na uvumilivu, kutakufanya kupoteza dira ya jambo husika kwa urahisi.....
Maadamu uko na nguvu tele usiogope kilima na makwazo wala mabonde unayoyapitia katika maisha yako ya kila siku.... tambua kwa kiasi kikubwa cha ugumu ndio unaoupitia basi tambua mbeleni kuna mafanikio makubwa....
Ogopa kuwa wa kawaida. Kila jambo ufanyalo ni la kawaida.. Inuka pambana, paza sauti yako, piga kelele, hakuna kukata tamaa mpaka uone umefika ufukwe wa mafanikio yako.... na ukishafika mwisho hakikisha unarusha kamba kwa jirani yako naye umtoe katika bahari ya umaskini na kuvusha kwenda ngambo au ufukweni kwa mafanikio.....
Nikutakie mapumziko mema
Br. Joseph Geotham Mrema

No comments
Post a Comment