KUWA MWANAHARAKATI WA MAISHA YAKO

KUWA MWANAHARAKATI WA MAISHA YAKO

Hellow watu wangu wa Nguvu, karibu tena katika makala hii fupi itakayokuongezea mwendo wa kuelekea ndoto zako.

Poleni na mihangaiko ya siku nzima na Hongereni pia....

Kwa wafanyakazi na waajiriwa kwa wafanyabiashara na wamiliki wa biashara kwa wenye ndoto na wasio na ndoto kwa wenye vipaji na wanaoona hawana vipaji....

Natamani kushirikiana na wewe jambo moja kabla hujalala....

Kwa kutambua kuwa wengi wetu humu ni wanaharakati wa maendeleo kwa namna moja au nyingine..

Harakati hizi zisizojali ukubwa wa ndoto au ukubwa wa umri au ukubwa wa mtazamo wako (hasi au chanya), pia sizisojali unamiliki wa jambo au haumiliku ila uko katika harakati hilo ndilo jambo la msingi...



Harakati za maendeleo hayo hasa katika kubadilisha maisha yetu ya kila siku

Katika mchakato mzima wa harakati za maendeleo, kuna kukatishwa tamaa na hata kukata tamaa hasa kutoka kwa watu waliokaribu nasi kwa namna moja au nyingine...

...muda mwingine watu hawa ni rafiki zetu wa karibu sana na wengine ni viongozi wetu ambao ulitegemea awe mhimili wa kuhakikisha lile jambo lako lafanikiwa kwa kiwango cha juu kabisa....

Maadamu umechagua kuvuka umechagua kutokuwa wa kawaida na waliokuzunguka ni lazima uwaze tofauti na waliokuzunguka, ni lazima utende zaidi ya waliokuzunguka, ni lazima uyatafute maarifa zaidi ya waliokuzunguka ili kuonyesha mapinduzi hali ya harakati zako....

Mwanafalsafa mmoja alisema

"Kujipangia malengo yasiyokutisha au kushangaza/kuwatisha watu, bado malengo yako ni ya kawaida sana ambapo mtu yeyote waweza yatimiza kwa wakati wowote"

Ni lazima kupanga yaliyo ya kiwango cha juu...

Kubali kuachana na kufanya mambo yaliyoya kawaida kawaida

Kubali kutafuta marafiki waliona mitazamo chanya hata waliokuzidi katika mambo mengi hasa ya kimaendeleo

Kubali kutafuta maarifa kwa namna yoyote (hasa katika vitabu na majarida)

Kubali kutokuwa mtu wa kawaida kawaida.

Mwisho;
Hakikisha unayafuata yake yaliyogusa moyo wako na sio yakiyovutiwa na macho yako....

Maana macho huona mengi ila moyo huguswa na machache mno....

Nikutakie siku njema Kijana mwenzangu....
_________________________________________________

Joseph Geotham Mrema
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc
Blog: Joche Motivates You
Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp&Calls: +255 (0) 712 851 687

No comments

Featured post

MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI

 MAMBO NANE YANAYOWAVUTIA WATEJA WENGI 1.Kuhudumiwa na Mtu anaye SMILES. Humfanya mteja ajihisi yuko huru zaidi kuuliza na kuamini unaweza k...