DHARAU ZA WANAJAMII ZISIKUPUNGUZIE MWENDO
DHARAU ZA WANAJAMII ZISIKUPUNGUZIE MWENDO
Habari?
Nakusalimu ndugu yangu rafiki, jamaa, kijana mwenzangu, mkubwa kwa mdogo...
Napenda kukukaribisha katika makala zetu ambazo ziko katika mlengo wa kukufundisha jambo, kukuonya, kukuonyesha, kukuhamasisha lakini pia kukuongezea maarifa ndani yako...
Katika maisha yetu ya kila siku kuna mambo ambayo hutokea muda mwingine tushayaona ni yakawaida kabisa lakini kiuhalisia si ya kawaida na muda mwingine hupoteza dira ya jamii au hata ya mtu fulani katika jamii hiyo
Katika Jamii kuna watu wa aina tofauti tofauti sana na utifauti huu ndio hufanya sote kutegemeana...
Mfano: kuna warefu na kuna wafupi, kuna wenye vipaji fulani na wengine wanavyo vya aina nyingine, kuna wengine wana utaalamu fulani na wengine hawana...
Haya yote hufanya jamiii iwe moja na kwa kutegemeana huku kila mtu akiheshimu alichonacho mwenzake basi jamii hiyo huendelea na kukua kwa maana kila mtu atathamini kile ambacho mwenzake anacho....
Maswali ya Msingi:
1. Je wewe katika jamii unayoishi una kitu gani/utaalamu gani/kipaji gani ambacho kinafanya jamii ikutegemee na kukutambua???
2. Je kama huna umewatia moyo kiasi gani wale ambao wanavyo?? Ili ujifunze kwao au waweze kusaidia maisha yako kwenda mbele zaidi???
Tatizo kubwa tulilonalo kama jamii ni kuona fulani hafai na fulani anafaa zaidi au kudharau wale ambao wanaweza kufanya jambo fulani endelevu katika jamii yetu ili kuhakikisha tunafisha au tunawavunja moyo wasisonge mbele....
Jamii ni kama familia wote yatupasa kuthaminiana na kutambua mchango wa kila mmoja wetu...
Usimdharau kwa vile amekuzidi kwa namna moja au nyingine au kwa vile nyota yake inang'aa zaidi katika kila jambo...
Mtie moyo, msaidie, mshauri, kwa sababu kuna wakati utahitaji huduma yake na utakosa kwa sababu ulidharau jambo lake...
Yawezekana ni Kanisani/ Msikitini/ Mtaani/Nyumbani/Mtaani....
Hawaoni mchango wako, hawaoni kujitoa kwako kwao, hawaoni gharama unazoingia kazi yao ni kudharau tu...
WEWE USIANGALIE HILO, INUKA SONGA MBELE mafanikio yako yako mlangoni mwako...
DHARAU ZAO NDIO MAFUTA YA GARI YAKO KUELEKEA MAFANIKIO...
Siku zote FANYA KWA VIWANGO hata kama hawataona mchango wako katika kile unafanya... ila wewe fanya kwa VIWANGO usiache doa popote....
MWISHO:
Kudharau, kutothamini jambo ambalo mtu analifanya hakutakufanya wewe ufanikiwe zaidi yake... Bali utakuwa unamuongezea speed ya kuelekea mafanikio yake huku akikuacha wewe ukiwa umembeba katika akili zako..
Thamini jamii yako, thamini utaalamu/vipawa/shughuli/biashara/kazi za wanajamii wenzio maana ndipo palipo na mafanikio yako...
Kujitenga na jamii yako hakukufanyi uweze kufanikiwa peke yako... Maana katika kuelekea mafanikio yako unahitaji watu... na watu watakao kuunga mkono ni wale wanakufahamu lakini kama ulidharau vya kwao, usitegemee wao watapenda vya kwako hata viwe katika Ubora wa Nyota 300...
Ndio maana kuna waliofanikiwa si kwasababu ya akili nyiiiingi, elimu kuuubwa, au vipawa vya hali ya juu... bali ni waliungwa mkono na jamii inayomzunguka maana aliithamini na yenyewe ikamthamini....
AMEN
_________________________________________________
JOSEPH GEOTHAM MREMA
Founder of Josel Company
Joche Inspirational and Motivational Inc
Visit us:
Facebook: Joseph Geotham Mrema
Instagram: joseph_geotham_mrema
Fb Page: Joche Talks
Blog: www.jocheinc.blogspot.com
Contacts Us:
Email: josephgeotham4@gmail.com
Whatsapp&Calls: +255 (0) 712 851 687
No comments
Post a Comment